loader
Tanzania yaridhia kuanza mchakato wa sarafu moja

Tanzania yaridhia kuanza mchakato wa sarafu moja

Mpaka wabunge wa Tanzania wanaridhia umoja huo Juni 25 mwaka huu, Tanzania ilikuwa ya kwanza kufanya hivyo na hakuna nchi nyingine iliyokuwa imeridhia ambapo mwisho wa kufanya hivyo ilikuwa Julai mosi mwaka huu.

Mkuu wa Mawasiliano serikalini katika Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Vedastina Justinian alisema iwapo nchi zote zitaridhia itakuwa imeruhusu kuanza kwa mchakato mrefu wa kuelekea sarafu moja kuanza.

Alisema mwaka jana wakuu wa nchi walisaini itifaki hiyo katika mkutano mkuu uliofanyika Kampala, Uganda na kupeana muda wa kila nchi kuridhia.

“Madhumuni ya umoja wa fedha ni kujenga ukanda tulivu wa kifedha wa jumuiya hiyo utakaorahisisha na kusaidia ukuaji wa biashara na shughuli za kiuchumi ndani ya jumuiya,” alisema.

Alisema manufaa yatokanayo na umoja wa fedha ni kupunguza gharama ya kufanya biashara katika nchi wanachama na hivyo kuhamasisha ukuaji wa biashara baina ya nchi wanachama.

Pia kuwezesha nchi wanachama kuwa na kiwango kidogo na tulivu cha mfumuko wa bei na kuwawezesha nchi wanachama kuwa na viwango vidogo vya riba ya kukopa.

Justinian alisema katika utekelezaji wa itifaki hiyo utafanyika hatua kwa hatua kwa kuzingatia mpango kazi ulioandaliwa na nchi wanachama na kufikia vigezo vilivyokubalika vya muunganiko wa uchumi mpana na masharti mengine yaliyoainishwa katika itifaki.

Alisema kwa kutambua kuwa nchi zote wanachama haziwezi kufikia vigezo hivyo na masharti mengine ya kuanzisha umoja wa fedha kwa wakati mmoja, na itifaki inaruhusu kwamba iwapo aghalau nchi tatu zitafikia vigezo na masharti mengine yaliyoainishwa zianzwe za kuanza kutumia sarafu moja.

WAKALA wa Usafi ri wa Mabasi ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko na Katuma Masamba

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi