loader
TGNP yaanzisha vituo vya taarifa, maarifa

TGNP yaanzisha vituo vya taarifa, maarifa

Ofisa Habari wa TGNP, Deogratius Temba alisema hayo mjini hapa alipokuwa akizungumza katika warsha ya siku mbili.

Warsha hiyo ililenga kuelezea uamuzi wa mtandao kuanzisha vituo vya taarifa na maarifa na kushirikisha waandishi wa habari 20 . Vituo vilivyoanzishwa viko katika kata za Mshewe, Ijombe na Tembela.

Moja ya kazi ya vituo hivyo ni kutoa na kutafuta taarifa wananchi wazipate kwa wakati.

“Wananchi wanaogopa viongozi wa vijiji na hivyo kutotoa taarifa, kwa mfano mwananchi haruhusiwi kuzungumza bila ya ruhusa ya mwenyekiti wa kijiji na wale wanaoonekana wanaongea sana wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria bila hata ya kuwa na kosa,” alisema.

Aidha Temba alisema kabla ya kuanzisha vituo hivyo, wanafundisha wananchi juu ya umuhimu wa kutoa na kupata taarifa na haki waliyonayo juu ya kuhoji vyanzo vya mapato ya kijiji, ruzuku waliyopokea kutoka serikalini pamoja na taarifa ya mapato na matumizi.

Baadhi ya waandishi wakizungumza katika warsha hiyo walisema uanzishwaji wa vituo hivyo utawasaidia kupata habari za vijijini kwa urahisi zaidi kupitia kwa viongozi wa vituo hivyo.

Charles Mwaipopo alisema vituo vya taarifa na maarifa vitakuwa ni daraja na vitakuwa ni vyanzo vya habari. Hadi sasa TGNP imefungua vituo 14 vya taarifa na maarifa vyenye kompyuta na intaneti.

MWENGE wa Uhuru unaendelea ...

foto
Mwandishi: Merali Chawe, Mbeya

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi