loader
Tigo waingia mkataba na Huawei

Tigo waingia mkataba na Huawei

Akizungumza na waandishi wa habari juzi, Mkuu wa Kitengo cha Takwimu na Vifaa vya Simu, David Zacharia amesema ushirikiano huu unawapa wateja fursa ya kuweza kumiliki simu ya Huawei Y330 kwa bei la punguzo ya Sh 130,000 na Huawei Y530 kwa sh 195,000.

Zacharia alisema wanunuzi wa simu hizo mbili watapata kifurushi cha bure cha thamani ya Sh 30,000 katika mwezi wa kwanza baada ya kununua kifurushi ambacho kinajumuisha dakika 600 za muda wa maongezi,ujumbe mfupi 8,000 za na GB 1.5 za data za intaneti.

Meneja Chapa wa kanda ya Afrika Mashariki na Kusini wa Huawei, Azalea Du alisema kwamba Huawei Y330 ni simu za kisasa zinazolenga vijana, ambayo kampuni yao inafarijika kuwapatia wateja wa Tigo fursa ya kuitumia.

foto
Mwandishi: Regina Kumba

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi