loader
Tozo yakimbiza watalii Makumbusho ya Mkwawa

Tozo yakimbiza watalii Makumbusho ya Mkwawa

Kwa mujibu wa mwongoza wageni wa makumbusho hayo, Zuberi Suleiman, wageni kutoka nje wanatakiwa kulipa Sh 20,000 kwa kichwa na Watanzania ni Sh 1,000, kitu ambacho alisema chaweza kuwa kikwazo kwa wageni.

Alisema kati ya wanaotembelea makumbusho hayo, asilimia 85 ni Watanzania.

“Wazungu wengi huishia nje ya lango hili baada ya kuambiwa gharama hiyo; zamani kila mzungu (watalii wa nje) alikuwa anaonekana ana pesa, kumbe hali ni tofauti kwa sasa hivi,” alisema.

Alisema, “wageni hao wanapotajiwa kiasi hicho cha fedha hushangaa na kuamua kuishia nje ya makumbusho na kuondoka.”

Hata hivyo Suleiman ameshauri makumbusho hayo yaboreshwe kuchochea utalii ili idadi iongezeke tofauti na sasa, ambapo hupokea wastani wa wageni 2,000 tu kwa mwaka.

Aidha, ameshauri tozo ya kuingia kwa lengo la kupata taarifa na kuona fuvu la chifu huyo lililohifadhiwa katika makumbusho hayo, ipunguzwe pawepo ongezeko la watalii.

Alikuwa akitoa taarifa kwa waandishi na baadhi ya maofisa wa Wizara ya Maliasili na Utalii waliofanya ziara kwenye makumbusho hayo.

Msemaji wa Wizara , Nurdin Chamuya aliyeongozana na waandishi wa habari, aliahidi kufikisha ushauri huo kwa Katibu Mkuu wa Wizara yafanyiwe kazi.

Aidha ameshauri maboresho mengine yawe ya kujenga kambi za kulala wageni, mgahawa, baa, bwawa la kuogelea. Pia amehimiza yatolewe matangazo hususani vipeperushi kutambulisha makumbusho hayo.

WADAU wa Sekta ya Kilimo nchini wameshauriwa ...

foto
Mwandishi: Frank Leonard, Iringa

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi