loader
TPA yajisogeza karibu na wafanyabiashara DRC

TPA yajisogeza karibu na wafanyabiashara DRC

Hatua hiyo imelenga kuwaondolea usumbufu wafanyabiashara wa nchi hiyo jirani, wanaotumia bandari ya Dar es Salaam, Hayo yalielezwa na Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe wakati wa uzinduzi wa ofisi ya mawasiliano ya TPA mjini Lubumbashi.

Aliongeza kuwa wizara yake na bandari ya Dar es Salaam, watahakikisha kuwa huduma za bandari zinasogezwa karibu na DRC. “Nawahimiza wafanyabiashara wa DRC kutumia kwa ufanisi ofisi hii kwa faida ya jamii nzima ya nchi yao,” alisema.

Mwakyembe alisema ofisi hizo mpya, zitasaidia wafanyabiashara wa DRC kumaliza matatizo yao Lubumbashi, badala ya kusafiri hadi Dar es Salaam.

“Wataweza kufanya malipo ya bandari wakiwa Lubumbashi na kuepuka hatari ya kusafiri na kiwango kikubwa cha pesa na kuibiwa,” alisema Mwakyembe.

Alisema tatizo lililokuwa linawakabili wafanyabiashara hao la kukabiliana na wakala wa kupakia na kupakua mizigo wasio waaminifu, sasa litakuwa historia, kwa kuwa ofisi ya Lubumbashi itakuwa na orodha ya wakala wanaokubalika na waaminifu.

Pia, mienendo ya taarifa za mizigo, itafanyika mjini humo, hivyo kuharakisha taratibu za mizigo bandarini hapo.

Mwakyembe alisafiri kwa barabara kwa zaidi ya kilometa 2,000 kutoka Dar es Salaam hadi Lubumbashi kupitia Zambia, kuangalia na kupata taarifa za changamoto wanazokumbana nazo wafanyabiashara wa DRC bandarini Dar es Salaam njiani wanaposafiri.

Ujumbe huo ulijumuisha pia maofisa waandamizi kutoka TPA, Mamlaka ya Usafiri wa Nchi kavu na Majini (SUMATRA), Kampuni ya Reli (TRL) na Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).

Ofisi ya Lubumbashi inalenga kuondokana na changamoto mbalimbali zinazowakumba wafanyabishara hao, zikiwemo ucheleweshaji, wizi, vikwazo visivyohusiana na kodi na wakala wa kupakia na kupakua mizigo wasio waaminifu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Peter Serukamba ambaye ni mmoja wa ujumbe wa Tanzania aliyesafiri na Waziri huyo, alisema hatua hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi zote mbili.

Aliishauri TPA kuweka wafanyakazi wenye moyo na uadilifu katika ofisi hiyo mpya.

Makamu Mkurugenzi Mkuu wa TAZARA, Saidi Sauko alisifu hatua hiyo, akisema itasaidia shirika lao kuongeza ufanisi wa kazi zao. Shirika hilo linahusika katika kusafirisha mizigo ya DRC kupitia reli ya TAZARA.

Mizigo ya DRC imekuwa ikiongezeka kwa asilimia 24 kwa mwaka tangu mwaka 2004.

Imeongezeka kutoka tani 155,611 hadi tani 1,117,249 mwaka 2013. DRC ni ya pili kwa kupitisha mizigo mingi katika bandari ya Dar es Salaam.

Mizigo ya DRC inachukua asilimia 25 ya mizigo yote ya nchi jirani, inayopita katika bandari

UKOSEFU wa elimu ya biashara, uthubutu na ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Lubumbashi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi