loader
Dstv Habarileo  Mobile
Tuendeleze upendo tuliouonesha wakati wa mfungo

Tuendeleze upendo tuliouonesha wakati wa mfungo

Pamoja na pongezi hizo, lakini mfungo huo ambao ulihitimishwa juzi, ulionesha picha nzuri katika jamii, ambapo upendo ulitawala na amani ilikuwepo katika jamii.

Pamoja na utulivu huo, pia jamii bila kujali itikadi za dini zetu, tulikuwa wamoja tukitakiana heri na hata kualikwa au kualika ndugu na jamaa, kushiriki futari pamoja.

Hayo ni mambo mema ambayo Watanzania siku zote tunajivunia umoja wetu na upendo.

Licha ya kuwa na makabila zaidi ya 120 nchini, lakini tunaishi kama ndugu wa mama mmoja kwa kuvumiliana na kuheshimiana, ingawa kuna mikwaruzo ya hapa na pale lakini inamalizwa kwa mazungumzo na kuendelea kushirikiana, lengo likiwa ni kujenga Tanzania yetu!

Hivyo basi tukiwa leo tunasherehekea sikukuu ya pili ya Idd el Fitr, hatuna budi kuendelea kuoneshana upendo ule, tuliouonesha wakati wa mfungo, na kamwe tusikubali kutumiwa au kutumika kama chombo cha vurugu au uchochezi wa kuvuruga amani na ushirikiano wetu.

Nasema hivyo kwa maana katika kundi hili kubwa la Watanzania, wapo pia wachache wasiotaka amani wala upendo uwepo, hivyo hutumia kila njia kuleta vurugu, au kugombanisha watu kwa misingi ya udini na ukabila, mambo ambayo kamwe tusiyakubali katika jamii yetu.

Mapema juzi, msemaji Mkuu wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba alisema jeshi lake limejipanga na kuweka ulinzi wa kutosha maeneo yote ili wananchi washerehekee salama sikukuu.

Kauli hiyo, ni dhahiri kwamba katika watu milioni takribani 44, wapo wachache wakorofi ambao kwa njia moja au nyingine wanaweza kuleta vurugu katika mikusanyiko ya watu wengi kama hii sikukuu. Hivyo ni vyema pamoja na jeshi la Polisi kutoa angalizo, lakini usalama wetu sisi wananchi uko mikononi mwetu.

Ni vyema sisi wenyewe kila mmoja, akawa mlinzi wa mwenzake kwa kuhakikisha anatoa taarifa kwenye vyombo vya usalama pale anapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa amani.

Tuendelee kupendana na kuheshimiana na pia kujenga tabia ya kuwafichua wahalifu ambao siku zote wao hupenda machafuko, vurugu au matatizo yatokee ambayo kwao ni neema.

Leo tunapoendelea kufurahi, ambapo baadhi yetu tumepata mialiko kwenye sikukuu hii kutoka kwa ndugu zetu, ni vyema tukafurahi pamoja na pia tukumbuke kula kwa kiasi na kunywa kwa kiasi na kuepuka ulevi, ambao mwisho wake ni madhara. Tukumbuke kuwa, ulevi na ulafi ni mambo yenye madhara katika jamii.

Hata kama umealikwa, kunywa kwa kiasi na ule kwa kiasi ili kuhakikisha usalama wako na wale utakaowaendesha, ikiwa unatumia usafiri binafsi hata ule wa umma.

Rai yangu pia kwa madereva, wazazi na vijana kufurahia sikukuu hii kwa amani na kwa kuzingatia sheria, kama wewe ni dereva hakikisha unafanya kazi yako kwa uaminifu na kamwe usinywe pombe na kuendesha.

Kwa vijana, tunafahamu leo ni sikukuu, wazazi wamewaruhusu kwenda kusherekea kwenye maeneo kama vile kwenye fukwe za bahar.

Ni wajibu pia wa mzazi, kuhakikisha watoto wenu wanarudi nyumbani kwa wakati na pia kufahamu walipo. Ili mwisho wa siku sote tumalize sherehe hii kwa amani na furaha na sio kwa huzuni au vurugu. Heri ya Sikukuu ya Idd el Fitr!

WIKI iliyopita umefanyika uzinduzi wa siku ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi