loader
'Tunahitaji muda zaidi kulipa madeni'

'Tunahitaji muda zaidi kulipa madeni'

Wafanyabiashara hao wamesema, pamoja na maafa makubwa waliyoyapata hawajaona viongozi wakuu wa serikali wakafika kuwafariji.

Aidha wamesema, wanahitaji muda zaidi wa kulipa madeni yao.

Hata hivyo mfanyabiashara mwingine Lucas Mushi alisema wameweza kuwasiliana na taasisi walizokopa fedha kuwaeleza hali halisi na wameambiwa wasubiri watajibiwa.

Alisema katika mazingira yao magumu wameomba kupewa muda wa nyongeza wa kurejesha mkopo na pia kuangaliwa kama inawezekana waweze kupewa mikopo mingine ili waweze kuinuka tena kibiashara.

Pia alisema wanashindwa kuelewa ni nini msimamo wa Serikali juu ya soko hilo kwa sababu viongozi wana kauli tofauti juu ya soko hilo.

Aidha alisema hata kama Serikali ilikuwa na mpango wa kuboresha soko hilo basi wangefanya hivyo kabla wafanyabiashara hawajajenga kwa fedha zao au watoe miaka kadhaa ili wafanye biashara kurejesha hali yao ya awali ya biashara ndipo ujenzi mwingine ufanyike.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa soko hilo la Mchikichini, Jumanne Kongogo, alisema hasara iliyopatikana ndio inasababisha malalamiko yote hayo.

foto
Mwandishi: Regina Kumba

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi