loader
Ukerewe waendelea kupokea walimu wapya

Ukerewe waendelea kupokea walimu wapya

Ofisa elimu wa sekondari wa wilaya hiyo, Sylvester Mrimi amemwambia mwandishi wa habari hizi kuwa idara hiyo imepangiwa walimu wapya 105, lakini waliofika na kupangiwa vituo vya kazi ni 91.

Alisema walimu wote walitakiwa hadi kufikia Aprili 7 mwaka huu, wawe tayari wamefika katika vituo vya kazi lakini hadi sasa walimu 14 hawajulikani walipo na kuongeza kuwa walimu hao wakifika watapokewa na kupangiwa vituo vya kazi.

Akifafanua Mrimi alisema idara yake yenye shule za sekondari 21 ina upungufu wa walimu 409, kati yao 226 wa sayansi na upande wa masomo ya sanaa kukiwa na upungufu wa walimu 185.

Katika hatua nyingine, halmashauri ya wilaya hiyo imetumia fedha za matumizi ya ofisi kuwalipa walimu wapya fedha za kujikimu.

Ofisa elimu ya msingi wa wilaya hiyo, Fidelis Munyogwa alisema awali idara yake ilipokea fedha ya malipo ya kujikimu ya siku nne ya walimu wapya wakati wanatakiwa kulipwa siku saba.

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka vijana wa ...

foto
Mwandishi: Jovither Kaijage, Ukerewe

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi