loader
Ulinzi waimarishwa uzinduzi mbio za Mwenge wa Uhuru

Ulinzi waimarishwa uzinduzi mbio za Mwenge wa Uhuru

Imesema hatua hiyo inakuja kutokana na ukweli kwamba mbio za Mwenge wa Uhuru nia yake ni kuendeleza amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.

Hayo yalibainishwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangala wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Bukoba juzi alipotoa tamko juu ya sherehe hizo za uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2014.

Alisema pia Serikali kupitia mbio za Mwenge imekuwa ikiwahamasisha wananchi, mashirika, taasisi na wadau mbalimbali kuchangia kwa hali na mali kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo.

Alisema Mwenge wa Uhuru uliasisiwa mwaka 1961 baada ya nchi kupata Uhuru kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza na tangu wakati huo umeendelea kuwa tunu na alama muhimu ya Taifa letu.

Alisema falsafa ya Mwenge huo ni kumulika ndani na nje ya mipaka ya nchi, kuleta matumaini ambapo hakuna matumaini, upendo mahali palipo na chuki na kuleta heshima palipo na dharau.

Alisema mbio za Mwenge mwaka huu zimebeba ujumbe usemao “Katiba ni Sheria Kuu ya Nchi, jitokeze kupiga kura ya maoni tupate Katiba mpya na pia ujumbe huo unaambatana na kauli za kuhamasisha kuhusu mapambano dhidi ya Ukimwi, matumizi ya dawa za kulevya, malaria na rushwa.

Alisema ujumbe kuhusu mabadiliko ya Katiba kwa mwaka huu umeandaliwa mahususi kwa ajili ya kuwahimiza wananchi kuendelea kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kutengeneza Katiba mpya iliyo bora zaidi unaoendelea hivi sasa ambapo mwisho wake ni wananchi kupiga kura ya maoni ili kupata Katiba mpya iliyoboreshwa kwa maendeleo ya Taifa.

Alisema mbio za Mwenge mwaka huu zitazinduliwa rasmi mjini Bukoba katika Uwanja wa Kaitaba Mei 2, mwaka huu ambapo mgeni rasmi Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal.

UJENZI  na ukarabati wa Soko la Kariakoo jijini ...

foto
Mwandishi: Angela Sebastian, Bukoba

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi