loader
Dstv Habarileo  Mobile
Upakuaji mizigo bandarini kuharakishwa

Upakuaji mizigo bandarini kuharakishwa

Upakuaji mizigo bandarini kuharakishwa Na James Gashumba, EANA-Kigali SERIKALI ya Tanzania imetangaza mipango mipya itakayorahisisha upakuaji wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam. Mipango hiyo ni ya kukarabati maeneo ya kupakulia mizigo kutoka moja hadi saba na kujenga maeneo mengine mapya manne ya aina hiyo kurahisisha upakuaji wa mizigo. Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania, Dk Harison Mwakyembe akizungumza katika mkutano wa Wakala wa Usafirishaji Mizigo (CCTTFA) uliofanyika mjini Kigali, Rwanda mwishoni mwa wiki kwamba Bandari pia imetenga eneo lililo karibu na bandari hiyo kwa lengo la kujenga bandari kavu kuhudumia shehena zinazosafirishwa kwenda katika nchi za Rwanda, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Dk Mwakwembe alifafanua kwamba kutokana na juhudi hizo mpya idadi ya siku za kusafirisha shehena kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda Rusumo, mpakani mwa Rwanda na Tanzania zitapungua kutoka siku 3.5 hadi 2.5. Makamu wa Rais wa Chama cha Madereva wa Magari Yaendayo Safari Ndefu nchini Rwanda (ACPLRWA), Issa Mugarura alisema wamekuwa wakihakikishiwa huduma hiyo na Serikali ya Tanzania wakati wote lakini utekelezaji bado ni changamoto. Hivi sasa Bandari ya Dar es Salaam inapokea shehena ya tani milioni 13.5 kwa mwaka na inatarajiwa kuongezeka na kufikia tani milioni 18 baada ya kukamilika kwa mabadiliko hayo mapya.

Sehemu kubwa ya ulimwengu wa biashara uli dorora kutokana na ...

foto
Mwandishi: James Gashumba, EANA-Kigali

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi