loader
UTT waanza kuuza vipande kupitia M-Pesa

UTT waanza kuuza vipande kupitia M-Pesa

Akizungumza juzi jijini Dar es Salaam, Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa UTT, Simon Migangala alisema ubia wa kutumia huduma ya M-pesa utapanua wigo wa UTT katika kuwafikia watanzania.

Alisema mifuko ambayo inaunganishwa na huduma hii ni mfuko wa Kujikimu, Watoto, Umoja na Wekeza Maisha.

Naye Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Salum Mwalim alisema M-pesa ina mawakala zaidi ya elfu 70 nchi nzima, hali ambayo itaisaidia UTT kuboresha biashara huku ikiwawezesha watanzania wengi zaidi kuwekeza katika mifuko hiyo.

Mwalim aliipongeza UTT kwa kuungana na mamia ya watoa huduma nchini ambao wameona fursa iliyopo kwa M-Pesa katika kurahisisha huduma na kupunguza gharama za uendeshaji na ufikiwaji wa huduma kwa upande wa wateja.

Alisema ukuaji wa M-Pesa umekua na manufaa makubwa kwa wananchi ambao sasa wana nafasi kubwa ya kukamilisha shughuli zao nyingi za kijamii na kiuchumi kupitia simu zao za mkononi.

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi