loader
Dstv Habarileo  Mobile
Uyole FC bingwa Kombe la Bodaboda

Uyole FC bingwa Kombe la Bodaboda

Uyole imekuwa bingwa wa mashindano hayo yaliyoandaliwa na Kampuni ya City Signs Agency ya hapa kwa udhamini wa Kampuni ya Coca Cola baada ya kuifunga Kabwe FC kwa mabao 2-0.

Katika fainali iliyochezwa kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge mbele ya Waziri wa Uchukuzi, Dk Harison Mwakyembe aliyekuwa mgeni rasmi, Kabwe FC walishindwa kumudu mchezo huo tangu mwanzoni.

Mabao yaliyofungwa na Miraji Juma katika dakika ya 41 na Baraka Agogo dakika ya 75, yalitosha kwa timu ya Uyole kutangazwa bingwa wa mashindano hayo yaliyoshirikisha timu za madereva wa bodaboda wote jijini hapa na pia Mji Mdogo wa Mbalizi uliopo katika Halmashauri ya Mbeya.

Kwa ushindi huo, Uyole imejinyakulia pikipiki aina ya Boxer yenye thamani ya Sh milioni mbili na kombe huku washindi wa pili, Kabwe ikizawadiwa Sh 700,000.

Timu ya tatu iliyojinyakulia Sh 300,000 ni Iyunga FC iliyoifunga mabao 3-0 Soweto FC, kwa mabao ya Salim Mvungu dakika ya 30 na Pinton Kwani dakika ya 70 na ya 76 katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu.

YANGA leo saa 1:00 usiku itashuka dimbani kuikabili ...

foto
Mwandishi: Joachim Nyambo, Mbeya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi