loader
Dstv Habarileo  Mobile
VETA, Wakenya kufundisha utalii

VETA, Wakenya kufundisha utalii

Makubaliano hayo yalifanyika jijini hapa leo baina ya Mkuu wa Vyuo vya VETA nchini, Zebadiah Moshi na Mkuu wa Chuo cha VETA Kenya, Dk Kenneth Ombongi.

Moshi alisema wakuu wa vyuo hivyo, wamekubaliana kuendesha mafunzo katika sekta ya hoteli na utalii kwa walimu ili waweze kufundisha vizuri wanafunzi wanaochukua masomo hayo.

Alisema soko la huduma za hoteli na utalii, linakua kwa kasi kubwa, hali inayosababisha ukosefu wa wahudumu wenye utaalamu wa hali ya juu wa kuhudumia hoteli za kitalii na kupelekea ajira kuwa za wageni pekee.

Alisema makubaliano hayo yatasaidia kupata uzoefu wa kubuni mbinu mpya za kupata wanafunzi bora wenye utaalamu wa juu na wa kati katika kuhudumia hoteli na sekta ya utalii ambayo inakuwa kwa kasi.

“Makubaliano haya yana faida kwetu kwani wenzetu wa Kenya wapo mbali sana katika sekta ya utalii na hoteli na nia ya Serikali kuanzisha chuo hiki Arusha na kuweza kupata wataalamu katika sekta hiyo na kusaidia kupata ajira kwani mahitaji ya watu hawa ni makubwa sana, na chuo hiki kimejipanga kukabiliana na soko la ajira.‘’ alisema.

HALMASHAURI ya Manispaa ya Morogoro imepata nmkopo ...

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Arusha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi