loader
Vijana wasiige visivyostahili

Vijana wasiige visivyostahili

Daktari wa Kitengo cha Matibabu ya Saratani, Hospitali ya Aga Khan, Dk Amiyn Alidina amenukuliwa na gazeti hili kuwa ulevi huo ambao kwa sasa umeshika kasi na kuteka watu wengi hasa vijana, una hatari kubwa kuliko uvutaji wa sigara.

Anaongeza kuwa kilevi hicho hakina tofauti na sigara, ambayo mvutaji wake hawezi kukwepa magonjwa kwani mbali na saratani, pia kuna athari ya maradhi ya moyo na maradhi ya mfumo wa hewa.

Shirika la Afya Duniani (WHO), pia limebainisha athari za kilevi hiki na kutanabaisha kuwa mkupuo mmoja wa shisha una kemikali hai 4,800 na kwamba kemikali hizo husababisha saratani ya mapafu, maradhi ya moyo na matatizo katika mfumo wa hewa.

WHO inaeleza kwamba, kiasi cha uvutaji wa shisha kwa saa moja ni sawa na kuvuta sigara kati ya 100 na 200 na hii inamaanisha kuwa mvutaji wa sigara hupata mikupuo kati ya minane na 12 ambayo huingiza lita 0.5 hadi 0.6 za moshi.

Lakini kwa upande wa shisha, anaweza kuvuta mara 200, kiasi ambacho huingiza kati ya lita 0.15 hadi moja ya moshi, katika mfumo wa mwili wake.

Ulevi huo hutengezwa kwa kutumia chombo maalumu chenye bomba la kutolea moshi, ambacho huwekewa tumbaku, maji na moto huku ikiaminika mvuke husaidia kuchuja nguvu ya tumbaku inayoathiri mwili.

Kwa hapa nchini kilevi hiki kimezidi kupamba moto kwenye klabu za usiku na watu wanaoonekana kuchagamkia kwa kasi ya kutisha ni vijana wa kike na wa kiume kwa imani kuwa wanakwenda na wakati.

Imani hii imejengeka kwa vijana kutokana na muundo wa mtungi wenyewe na pia shisha kuwa na ladha mbalimbali zinazowavutia watumiaji kuliko ilivyo kwa ladha ya sigara.

Hali ya ongezeko la uvutaji wa kilevi cha shisha unakuwa hapa nchini hususan kwa vijana kwa sababu hawajui hatari ya kilevi hicho na wengi wamekuwa waigaji wakiamini ndio maisha ya kisasa.

Wakati ukweli wa mambo ni kuwa kilevi cha shisha kina ladha tofauti na sigara, lakini tumbaku hiyo ina sumu ya toxin ambayo iko kwenye tumbaku ambayo husababisha kansa ya mapafu na ugonjwa wa moyo.

Pamoja na watumiaji kuamini kuwa moshi huo ambao hupitia kwenye maji hivyo kemikali za sumu zilizomo hufyonzwa na maji hayo, imani hii ni potofu na haina ukweli wowote.

Ukweli ni kuwa uvutaji huu unamfanya mtumiaji kuingiza kemikali kwa wingi katika mfumo wa hewa.

Lakini pia hata kwa afya ya mvutaji wa kilevi hiki cha shisha huwa matatani, katika hali ya kawaida haiwezekani mrija mmoja ukatumika kwa watu zaidi ya mmoja na wengi wao hupokezana.

Kuchangia huku kunaweza kuchangia maambukizo mengine hususan ugonjwa wa kifua kikuu.

Ili kupambana na hali hiyo, ni vyema wamiliki wa baa na klabu za usiku ambazo zimeanzisha uvutaji wa aina hii, kuhakikisha wanaweka onyo kwenye mitungi hiyo ili kueleza madhara yatokanayo na uvutaji huo.

Hii itamfanya mtumiaji kujua anachokifanya kama ilivyo kwa sigara.

Pia vijana wetu wanatakiwa kuacha tabia ya kuiga visivyoigika na kuepuka matumizi ya kilevi.

JUMUIYA ya Afrika Mashariki (EAC) inazidi kuimarika.

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi