loader
Dstv Habarileo  Mobile
Vitendo vya ukatili kwa watoto vyaongezeka

Vitendo vya ukatili kwa watoto vyaongezeka

Hayo yamo katika taarifa ya Kituo cha Haki za Binadamu Tanzania (LHRC) kwa mwaka 2013 iliyozinduliwa jana Dar es Salaam.

Akizungumzia ripoti hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk Hellen-Kijo Bisimba alisema kituo hicho kinasikitishwa kudorora kwa haki za binadamu hasa suala haki za mtoto kuonekana kuwa tishio.

“Watoto wengi hawawezi kujitetea na bahati mbaya matukio ya watoto kufanyiziwa vitendo viovu na walezi wao wakiwemo wazazi na hata walimu vimeongezeka,” alisema Dk Hellen.

Alisema kutokana na kuongezeka kwa vitendo hivyo ipo haja ya kuanzishwa shule za kutoa elimu kwa wazazi na walezi juu ya njia bora na sahihi za kulea watoto na kwa wale wanaofanya vitendo vya kikatili ipo haja ya kuhakikisha wanachukuliwa hatua zinazostahiki kwa mujibu wa sheria.

Akifafanua zaidi kuhusu matukio ya ukatili kwa watoto, Pacience Mlowe kutoka LHRC, alisema watoto wameendelea kuishi katika mazingira magumu nchini ambapo haki zao msingi hazitekelezwi na wale wanaotakiwa kuwasimamia na kuwalinda.

Alisema baadhi ya matukio ya ukatili kwa watoto ambayo yameripotiwa katika vyombo vya sheria kuanzia Januari hadi Desemba mwaka jana ni pamoja na watoto 250 kutelekezwa, watoto kuasiliwa 142, waliolawitiwa 863 na kunajisiwa matukio 10.

Kuhusu watu kuuawa kwa wananchi kujichukulia sheria mkononi alisema pia ni vitendo ambavyo vimeongezeka kwa kasi ambapo kwa mwaka jana watu 1,669 waliuawa nchini huku Dar es Salaam ikiua 240.

Alisema mauaji mengine yalitokana na watu kuuawa na vyombo vya dola, mauaji ya raia dhidi ya polisi ambapo polisi wanane waliripotiwa kuuawa na raia.

Akizindua taarifa hiyo, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Isaya Mngulu alisema ukatili wa kijinsia ni suala ambalo bado linazidi kushamiri na kuitaka jamii kubadilika na kuwa walinzi wa wao wenyewe.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania alisema watu kujichukulia sheria mikononi limekuwa suala la kawaida, jambo linalosababisha watu kuendelea kukatishia uhai.

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi