loader
Viwanja vya Sabasaba sasa kujengwa upya

Viwanja vya Sabasaba sasa kujengwa upya

Katika awamu awamu ya kwanza, baadhi ya majengo yatabomolewa na kujengwa upya. Majengo ya taasisi mbalimbali yatabomolewa na kujengwa kumbi za mikutano, mabanda ya kisasa kwa ajili ya maonesho na hoteli ya kisasa.

Mkurugenzi wa TanTrade, Jacqueline Maleko alisema hayo wakati wa kufunga Maonesho ya 38 ya Kimataifa yaliyofanyika kwa siku 10 na kumalizika juzi katika viwanja hivyo.

Alisema wanatekeleza agizo la Waziri Mkuu Mizengo Pinda alilotoa alipotembelea maonesho hayo wiki iliyopita. Pinda alisema washiriki wa maonesho hayo wameongezeka hivyo ni vyema majengo yakabomolewa na kujengwa upya, kwani eneo hilo siyo la kisasa kwa maonesho ya kimataifa.

“Katika mwaka huu wa fedha tumedhamiria kuanza kuboresha miundombinu ya eneo hili la maonesho kwa awamu ya kwanza, kwa kujenga kumbi za mikutano, mabanda ya maonesho ya kisasa na hoteli kubwa,” alisema Maleko.

Alisema changamoto iliyojitokeza katika maonesho ya mwaka huu ni kuchelewa kwa vitambulisho kwa washiriki wengi, jambo lililosababishwa na upya wa utoaji wa vitambulisho hivyo, ambavyo siyo rahisi kughushiwa.

Alisema jambo kubwa kwa mwaka huu ni kufanikiwa kuweka kamera za CCTV na kuangalia usalama kwa watu wote, wanaoingia na kusaidia kudhibiti vitendo vya wizi.

Alisema kuanzia sasa kanuni za kufanya maonesho mbalimbali nchini zimetoka; na Tantrade imepewa kazi ya kusimamia maonesho yote nchini. Hivyo hakuna anayeweza kufanya maonesho bila kibali chao.

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi