loader
Vodacom kuboresha M-pesa

Vodacom kuboresha M-pesa

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Rene Meza alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia mafanikio yaliyopatikana kutokana na huduma ya M-pesa.

Alisema tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo ya kifedha mwaka 2008, kampuni ina mawakala 70,000 wa huduma hiyo ya kutuma na kupokea fedha kwa wateja wake zaidi ya milioni 27.

“Tuko katika mazungumzo na watoa huduma wengine wa fedha kupitia njia ya mitandao kuangalia namna ambavyo tunaweza kuboresha huduma hii zaidi,” alisema.

Hata hivyo, alisema wako katika ushirikiano na benki zaidi ya 26 nchini ambazo zimeunganishwa na huduma hiyo ya kifedha inayowezesha wateja kutoa fedha au kuweka moja kwa moja kwenye akaunti zao.

Alisisitiza: “Huduma hii ya M-pesa imekuwa na mafanikio makubwa katika kubadili maisha ya Watanzania, na siyo tu katika kutuma na kupokea pesa bali imekuwa na mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi yetu kutokana na kuwaweka mamilioni ya Watanzania katika mzunguko wa huduma za kifedha.”

WADAU wa Sekta ya Kilimo nchini wameshauriwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi