loader
Waagiza mapendekezo ya Tume Nansio kufanyiwa kazi

Waagiza mapendekezo ya Tume Nansio kufanyiwa kazi

Madiwani hao wametoa azimio hilo jana baada ya kupokea taarifa ya tume iliyoundwa Februari mwaka huu kuchunguza tatizo sugu la maji linaloukabili mji wa Nansio kwa miaka kadhaa sasa.

Mmoja wa madiwani hao, Ally Mambile mbali ya kuridhika na taarifa hiyo pia ametaka mapendekezo yote 28 yaliyopendekezwa na tume hiyo yatekelezwe kwa wakati ili kuondoa tatizo hilo.

Alisema pamoja na changamoto zilizopo za kitaalamu na kifedha, lakini wakazi wa mji wa Nansio kwa miaka zaidi ya mitatu iliyopita wanaishi katika mazingira magumu na hatari kwa afya zao kwa kukosa huduma ya maji.

Naye diwani wa kata ya Kakerege, Juma Mazigo alisema mbali ya madhara wanayopata wananchi pia mamlaka ya maji inaelekea kushindwa kutimiza wajibu wake baada ya mapato yake kushuka.

Alisema mamlaka hiyo iliweza kukusanya Sh milioni nne kwa kila mwezi kutoka ankra za maji, lakini hivi sasa mapato hayo yameshuka ambapo kwa mwezi zinakusanywa fedha isiyozidi Sh 900,000 baada ya wateja wengi kukosa huduma ya maji hivyo kuacha kulipa.

UJENZI  na ukarabati wa Soko la Kariakoo jijini ...

foto
Mwandishi: Jovither Kaijage, Ukerewe

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi