loader
Wabunge:Ugaidi Kenya hatari kwa utalii

Wabunge:Ugaidi Kenya hatari kwa utalii

Akichangia kwenye mjadala huo jana, Mbunge wa Viti Maalumu, Cynthia Ngoye (CCM), alisema mashambulizi ya kigaidi yanayofanyika nchini Kenya, yataathiri sekta ya utalii nchini.

Mbunge huyo alisema takwimu zinaonesha kuwa asilimia 40 ya watalii huingia nchini kupitia mpaka wa Namanga, hatua inayodhihirisha kuwa wapo watalii ambao huingia nchini wakitokea Kenya.

Ngoye alisema kwa sasa badhi ya watalii waliokuwa waje nchini, wameshaanza kusitisha safari zao kutokana na mashambulizi hayo.

Kutokana na hali hiyo, Mbunge huyo alitaka Serikali kuwa makini katika hatua zozote za kuongeza kodi katika sekta ya utalii. Kuhusu kuongeza wigo wa mapato, Ngoye alitaka Serikali kuangalia uwezekano wa kutoza kodi wamiliki wa nyumba za kupanga, kiwe chanzo kipya cha mapato.

“Mheshimiwa Spika wakati umefika sasa kwa wamiliki wa nyumba za kupanga kutozwa kodi. Tukikitumia chanzo hiki vizuri Serikali itaweza kupata fedha nyingi na kujiongezea mapato,” alisema.

Kwa upande wake Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), alieleza kushangaa sababu za Serikali kutotaka kuchukua mapato kutoka katika sekta ya uvuvi katika bahari kuu.

Alisema Serikali iliwahi kufanya utafiti na kubaini karibu dola za Marekani milioni 222 zimekuwa zikipotea kila mwaka, kutokana na kukosekana kwa udhibiti wa uvuvi katika bahari kuu.

Hata hivyo, katika utafiti huo, Hamad alisema Serikali ilieleza imekuwa haipati mapato kutoka katika uvuvi wa bahari kuu kwa kuwa haina bandari ya meli za uvuvi, na kama wakiamua kuanza kutoza kodi, kuna uwezekano wa wawekezaji kuondoka, sababu alizosema si za kweli.

Alisema inashangaza kuona kuwa wakati Serikali ikihangaika kupata mapato yatokanayo na leseni katika meli chache za uvuvi, zipo meli zaidi ya 360, zinavua katika bahari kuu mamia ya tani za samaki bila kibali.

Kwa mujibu wa Hamad, wataalamu wa Serikali waliwahi kushauri kufanyike mnada wa kimataifa, ili wavuvi waje na malengo yao na Serikali iwapangie tozo zake ili kupata mapato stahiki lakini, ushauri huo haukuwahi kufanyiwa kazi.

Mbunge huyo pia aliitaka Serikali kuwa makini na uendelevu wa sera na miradi yake, akitolea mfano wa mipango na sera za Serikali katika kilimo.

Alisema bajeti ijayo ya 2014/2015, inaonesha kuwa kipaumbele kikubwa ni elimu, hivyo akataka Serikali kueleza inatarajia kupata wanasayansi wangapi na katika muda gani na wahandisi wangapi.

Kwa upande wake Mbunge wa Kawe Halima Mdee (Chadema) akichangia jana alisema kazi ya upinzani si kusifu Serikali, bali ni kukosoa utendaji wa Serikali na idara zake zote na kazi ya pili ni kutoa mawazo mbadala.

Alisema hata punguzo la kodi ya mshahara (PAYE), kwa wafanyakazi kutoka asilimia 13 katika mwaka unaoisha wa fedha, mpaka asilimia 12 katika mwaka ujao wa fedha limetokana na shinikizo kutoka Kambi Rasmi ya Upinzani, akidai ilikuwa ni hoja yao ya siku nyingi.

Akichangia juzi jioni Mbunge wa Viti Maalumu, Leticia Nyerere (Chadema) aliwataka wabunge wenzake wakiwemo wa Kambi Rasmi ya Upinzani, wanapoikosoa Serikali kwa kutokusanya kodi vizuri, wajiulize kama nao wanalipa kodi.

Nyerere aliisifu Serikali kwa kutoa huduma za kijamii zikiwemo za maji katika Jimbo la Kwimba, Mwanza anakotoka na kufafanua kuwa, anaposema ukweli kuhusu mambo yaliyofanywa na Serikali, kuna baadhi ya wenzake wa upinzani hawafurahi.

AS Tanzania celebrates its 60th anniversary of independence on ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi