loader
Wacanada wa methano wataka kuwekeza Tanzania

Wacanada wa methano wataka kuwekeza Tanzania

Imesema hiyo inatokana na Tanzania kuwa na hazina kubwa ya gesi asilia.

Hayo yamesemwa Makamu wa Rais wa kampuni ya Methanex kwa upande wa Amerika Kaskazini, Kevin Handerson wakati alipokuwa akizungumza na ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga uliofika katika kiwanda hicho kilicho katika jimbo la Alberta nchini Canada ikiwa ni sehemu ya ziara ya mafunzo kuhusu usimamizi na uendelezaji wa tasnia hiyo.

Handerson alisema uzalishaji wa methano utakuwa na manufaa makubwa kwa Tanzania kutokana na malighafi hiyo kutumika katika kutengeneza vifaa vya plastiki, gesi inayotumika majumbani, kutumika kwenye vyombo vya usafiri, viwanda vya kutengeneza rangi, viwanda vya mbao, kuzalisha umeme, kusafishia maji.

“Pamoja na Tanzania kuwa ni eneo muhimu kwa uwekezaji wa viwanda hivi vya kuzalisha methano ni muhimu Serikali ikatenga eneo maalumu kwa ajili ya uwekezaji wa namna hii, na kuzingatia uwepo wa sera, sheria, kanuni madhubuti zinazoongoza sekta hii, pia kuwe na miundombinu imara ya usafirishaji, maji, umeme wa uhakika pamoja na uwepo wa rasilimali watu,” alisema Handerson.

Akieleza kuhusu uwezo wa kampuni hiyo, Makamu Rais wa Methanex alisema kampuni hiyo ina uwezo wa kuzalisha tani milioni 8.5 za methano kwa mwaka na husafirisha malighafi hiyo katika sehemu mbalimbali duniani ikiwamo Hongkong, Shanghai, Beijing (China), Seoul (Korea Kusini), Tokyo (Japan) na Ubelgiji.

Vilevile Handerson alieleza kuwa kampuni hiyo ya Methanex ipo tayari kuja kuwekeza nchini Tanzania kwa kuwa wana uzoefu wa zaidi ya miaka 40 katika uwekezaji wa viwanda hivyo na wana mfumo mzuri wa kutoa mafunzo kwa wazawa ili kushiriki katika miradi ya methano.

Naye Kitwanga aliikaribisha kampuni hiyo kuja kuwekeza nchini Tanzania kwa kuwa kuna kiasi kikubwa cha gesi asilia cha zaidi ya futi za ujazo trilioni 50 ambazo pamoja na kutumika kuzalisha umeme pia inaweza kutumika kwa shughuli nyingine za kiuchumi ikiwamo kutengeneza methano na mbolea.

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalumu, Alberta, Canada

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi