loader
'Wachimbaji wadogo kopeni TIB'

'Wachimbaji wadogo kopeni TIB'

Alisema hatua hiyo itaenda sambamba na kupata masoko ya uhakika na bei iliyokuwa bora kwa wazalishaji hao wa madini.

Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Kusini Benjamini Mchwampaka aliyasema hayo leo wakati alipokuwa akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu, jasi, wazalishaji wa chumvi na madini ya ujenzi, kutoka katika mikoa ya Lindi, Mtwara na Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.

Alisema kutokana na kushindwa kuongezea thamani madini hayo, vipato vimekuwa vidogo na kuathiri hata ulipaji wa leseni na kusababisha ukwepaji mkubwa wa ushuru wa mamlaka mbalimbali.

Mchwampaka alisema kwamba mfano wazalishaji wa madini ya chumvi wanazalisha chini ya viwango mfano chumvi haijasindikwa na haijawekewa madini ya joto hatimaye wanauza chini ya bei ya Sh 1,500 mpaka Sh 2,000 kwa mfuko wa kilogramu 50.

Aliongeza kuwa kama mchimbaji angeweza kusindika kwa mashine na kuweka madini ya joto pakiti moja ya chumvi ya gramu 200 ingeuzwa kwa Sh 300, sawa na kuuza kiroba kimoja kwa Sh 75,000.

Kamishna huyo Msaidizi alisema kwamba hali si nzuri kwa wazalishaji wa madini ya chumvi kwani wanashindwa hata kulipia leseni zao kutokana na kushindwa kuzalisha kwa wingi na kuuza kwa bei nzuri.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Abdallah Chikota alisema kama wachimbaji wadogo watatumia fursa ya kupata mikopo kupitia Benki ya TIB ili kuwa na mitaji ya kutosha hawataweza kuboresha shughuli zao.

WAKALA wa Usafi ri wa Mabasi ...

foto
Mwandishi: Kennedy Kisula, Lindi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi