loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wafanyabiashara Dodoma waunda shirikisho

Wafanyabiashara Dodoma waunda shirikisho

Masoko mengine ni Chikanda, Stendi Kuu ya mabasi yaendayo Mikoani, Jamatini na One Way. Kumeelezwa kuwa kuwapo kwa shirikisho hilo kutawawezesha kufanya biashara zao kwa kufuata taratibu na sheria.

Akizungumza baada ya kuundwa kwa shirikisho hilo Mwenyekiti wa Umoja huo Norbert Pangaselo, alisema kuwa umoja huo utawawezesha kuwa na sauti ya pamoja hasa kero zinazowakuta katika biashara.

Aidha alisema umoja huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa migogoro ndani ya maeneo ya wafanyabiashara na kuwa kiunganisho kikubwa kati yao na serikali.

Mmoja wa wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao za kibiashara Juma Ibrahim alisema anatarajia shirikisho hilo kutoa elimu kwa wafanyabiashara kuacha kufanya shughuli hizo maeneo yasiyoruhusiwa.

Naye Katibu wa shirikisho hilo Sakina Said, amewataka wafanyabiashara wa masoko kutoa ushirikiano kwa chombo hicho ambacho kitakuwa ni msaada mkubwa kwao.

Sehemu kubwa ya ulimwengu wa biashara uli dorora kutokana na ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi,Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi