loader
Wafanyabiashara nchini waaswa

Wafanyabiashara nchini waaswa

Utumiaji wa rajisi hiyo, umeelezwa kuwa na manufaa makubwa kwani wateja wanaopata huduma kupitia mitandao hiyo, huwa na uhakika na huduma inayotolewa.

Aidha unaelezwa kuwa rajisi hiyo ina uwezo mkubwa wa kupambana na uhalifu unaofanywa katika mitandao, kupitia .tz information centre inyohusika na usajili wa rajisi.

Akizungumzia suala hilo katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendejea, Mhasibu wa .tz information centre, Peter John, alisema, bado watu wengi hawana uelewa wa umuhimu wa .tz.

“Moja kati ya faida hizo ni kukabiliana na uhalifu ambao kwa sasa umeshika kasi kubwa, endapo utapokea ujumbe kwenye barua pepe yako na ikaonyesha ina rajisi ya .tz uwezekano wa kumpata mtu aliyefanya uhalifu ni mkubwa,” alisema.

Alisema mbali na usalama anaopata mteja mwenye rajisi hiyo, lakini pia gharama zake ziko chini. “Unajua unapotumia rajisi za kijamii ni rahisi zaidi kuibiwa lakini pia huna pa kwenda kulalamika, lakini ukiwa na rajisi ya .tz ni vigumu sana kwa wewe kuibiwa,” alisema.

WAKALA wa Usafi ri wa Mabasi ...

foto
Mwandishi: Katuma Masamba

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi