loader
Wafanyabiashara sasa wachangamkia EFDs

Wafanyabiashara sasa wachangamkia EFDs

Akizungumza wakati wa utoaji wa elimu inayoendelea katika Maonesho ya Wakulima (Nanenane) mkoani Lindi, Ofisa elimu kwa walipa kodi mkoani humo, Julius Mafuru alisema sasa mwitikio wa kununua mashine hizo umeongezeka tofauti na awali wafanyabiashara walipokuwa wakizigomea kutokana na kukosa elimu.

Mafuru alisema changamoto waliyokuwa wakikumbana nayo ni baadhi ya watu kudai kuwa mashine hizo hazina uwezo wa kufanya kazi pindi umeme unapokatika na kwamba mashine hiyo haina uhusiano wowote kwani umeme unapokatika bado anakuwa na uwezo wa kuendelea kuitumia.

“Zamani walikuwa wakidai hawezi kutumia mashine za EFDs kwa madai kwamba umeme unapokata wanashindwa kuzitumia…lakini mashine ina uwezo wa kukaa na chaji ndani ya saa 48 hivyo haiwezi kumkwamisha mteja kufanya kazi zake,” alisema Mafuru.

Aidha Mafuru alisema mfanyabiashara anayetumia mashine hizo inamrahisishia kufanya biashara, ikiwa ni pamoja na kuweka na kuhifadhi kumbukumbu zake na sio kwa faida ya serikali pekee pia inaokoa muda wake wa kufanya hesabu.

“Tunawahimiza waendelee kutumia mashine hizo si kwa ajili ya wananchi na serikali pekee, bali hata kwa ajili yake inamsaidia kuhifadhi kumbukumbu na kuokoa muda wa kufanya hesabu zake,” alisema.

MGODI wa kati wa madini ya dhahabu ...

foto
Mwandishi: Clarence Chilumba, Lindi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi