loader
Wafanyakazi Dodoma wakemea matusi rasimu mpya ya Katiba

Wafanyakazi Dodoma wakemea matusi rasimu mpya ya Katiba

Kauli hiyo ilitolewa mjini Dodoma jana na Mratibu wa Sherehe za Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) kwa Mkoa wa Dodoma, Ramadhani Mwendwa katika sherehe zilizofanyika katika Uwanja wa Jamhuri.

Alisema msimamo wa wafanyakazi umekuwa siku zote muundo wa Serikali moja kwa kuwa hawataki kuwepo kwa mvutano wa madaraka ila wapo tayari kusikiliza mijadala mipana ndani ya Bunge hilo.

Alisema badala ya kushughulika na mambo muhimu yanayohusu maisha ya Watanzania, wajumbe wanasiasa wamegeuza Bunge kuwa kituko kwa kauli zao za matusi.

“Tunachowataka waache matumizi mabaya ya muda ambayo yanapoteza fedha nyingi za Serikali wakati yapo matatizo mengi katika sekta mbalimbali nchini,” alisema Mwendwa.

Kwa upande wake, Mgeni rasmi katika sherehe hizo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Rehema Nchimbi alisema Katiba inayoandikwa sasa lazima ijali maslahi ya wafanyakazi.

Dk Nchimbi aliwataka wafanyakazi kutambua kwamba wanamchango mkubwa katika kuhakikisha amani na utulivu uliopo nchini hauchezewi.

Katika sherehe hizo zilizoambatana na maandamano wafanyakazi katika risala yao pia wamelalamikia malipo madogo ya mshahara ambayo yanafanana na posho ya siku moja ya baadhi ya viongozi wa Serikali na taasisi mbalimbali.

Alisema pamoja na kilio cha wafanyakazi hao kutaka kupandishwa kwa kima cha chini cha mshahara hadi kufikia Sh 315,000 serikali bado haijatekeleza haja hiyo.

“Kima cha chini cha mshahara wa mfanyakazi kinamtosha kuishi kwa muda wa siku saba tu halafu ziku 23 zinazobaki anaishi kwa kukopa. “Mshahara huo ambao mfanyakazi anaupata kwa muda wa mwezi mmoja unalingana na posho ya siku moja ya baadhi ya viongozi wa Serikali au taasisi mbalimbali,” alisema.

Alisema pamoja na mshahara huo mdogo wafanyakazi hao bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kupanda kwa gharama za umeme na mafuta hali inayosababisha gharama za maisha kuwa juu.

Mwendwa alisema wafanyakazi wanaitaka Serikali kudhibiti matumizi ya fedha za Serikali ikiwemo ubadhirifu na rushwa ili Serikali iweze kupata mapato badala ya kutegemea kodi kutoka kwa wafanyakazi.

“Licha ya wafanyakazi kulalamikia makato makubwa ya kodi Serikali haijafanya jitihada za kupunguza wakati huohuo makampuni makubwa yanakwepa kodi na misamaha ya kodi inaongezeka kila siku,” alisema.

Alisema pia wafanyakazi hao wanaitaka Serikali kulipa madeni sugu ya wafanyakazi kwa kuwa iwapo yatapewa kipaumbele madeni hayo yote yatakwisha.

Katika hatua nyingine wafanyakazi hao wamelalamikia baadhi mifuko ya hifadhi ya Jamii kutokana na kutoa malipo kidogo ya mafao kwa wanachama wao.

Mbali na mifuko hiyo pia wameulalamikia Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) kuwa kutoweka baadhi ya dawa katika bima hiyo na kuweka madaraja ya matumizi ya kadi za mfuko huo.

UJENZI  na ukarabati wa Soko la Kariakoo jijini ...

foto
Mwandishi: Sifa Lubasi, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi