loader
Wafanyakazi wagomea utitiri wa serikali

Wafanyakazi wagomea utitiri wa serikali

Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Adelgunda Mgaya alisema hayo jana bungeni na kuongeza kuwa mazungumzo baina ya vyama vya wafanyakazi na serikali tangu 2006 yalisimamia nyongeza hiyo, lakini mpaka sasa haijatekelezeka hivyo kuongeza serikali ya tatu, ni kuzidisha maisha duni kwa wafanyakazi.

Mgaya alisema hayo wakati akichangia mjadala wa Rasimu ya Katiba mpya kuhusu sura ya kwanza na ya sita bungeni mjini Dodoma.

Mgaya alisema msimamo wa wafanyakazi nchini ilikuwa ni serikali moja, lakini kwa kuwa maoni ya wengi si serikali moja kwa sasa, ni bora kubaki na serikali mbili lakini iliyoboreshwa kwa kuweka vizuri maisha ya wafanyakazi ambao ndio wanaoumia kwa kukatwa kodi wakati mishahara yao ikizidi kuwa duni.

“Tunataka serikali itakayoboresha maisha ya wafanyakazi, itapandisha mishahara, itashusha kodi, itaboresha mazingira ya kazi kwani ni mabovu, unakuta daktari amesomeshwa vizuri anafika kazini hana vifaa wala dawa za kumpa mgonjwa, mwalimu anawafundisha watoto walioketi chini mpaka anapinda mgongo,” alisema Mgaya.

Alisema mazingira bora hayatokani na utitiri wa serikali, bali muendelezo wa mazungumzo baina ya serikali na vyama vya wafanyakazi kupitia Baraza la Utumishi wa Umma kwamba serikali ibane matumizi, wafanyakazi wapate mishahara mizuri.

“Tupo kwenye meza ya majadiliano, hatujafika kwenye lengo la kima cha chini cha Sh 315,000 tangu mwaka 2006 hadi leo, mzigo wa serikali upo mabegani mwa wafanyakazi kwa makato ya kodi, tunataka kodi ifikie kwenye ‘single digit’ (chini ya asilimia 10) lakini sasa ni asilimia 13, serikali tatu haitupeleki kwenye ‘single digit bali mzigo zaidi,” alishauri Mgaya.

Alisema ni bora kubaki kwenye serikali mbili itakayoboreshwa, ili kero zishughulikiwe na alishauri mambo makuu matatu katika rasimu akitaka kuwe na Tume ya Kudumu ya Kushughulikia Kero za Muungano, sura ya ardhi na kuwepo kwa usawa wa jinsia kama Tunu za Taifa.

“Usawa wa jinsia hatuutafuti bali ulikuwepo tangu uhuru, ukiangalia nembo yetu ya Taifa ina mwanamume na mwanamke, mfumo dume hapa katikati ndio umenyang’anya haki, tunaitaka irejee kama tunu,” alishauri Mgaya.

AS Tanzania celebrates its 60th anniversary of independence on ...

foto
Mwandishi: Waandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi