loader
Wafanyakazi watatu wa NMB kizimbani

Wafanyakazi watatu wa NMB kizimbani

 

Washitakiwa hao ni mfanyakazi wa benki hiyo, Mtoro Suleiman, Daudi Kindamba na John Kikopa. Walifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka hayo na Wakili wa Serikali, Pius Hilla, mbele ya Hakimu Mkazi, Hellen Riwa.

Hilla aliwasomea washitakiwa hao mashitaka ya kula njama, kuiibia benki hiyo Sh 1,029,454,383, kwa njia ya udanganyifu, kutakatisha fedha na kuisababishia benki hiyo hasara hiyo.

Inadaiwa katika tarehe tofauti kati ya Januari Mosi, 2007 na Julai 30, 2009 katika makao makuu ya benki hiyo, Dar es Salaam kwa udanganyifu na bila haki waliiba kiasi hicho cha fedha.

Hilla alidai Mtoro akiwa mtumishi wa benki hiyo aliingiza maingizo yasiyo sahihi katika akaunti maalumu na kuhamisha Sh milioni 579.8 kwenda akaunti binafsi ya Kindamba.

Pia anadaiwa kuhamisha Sh milioni 389 kutoka akaunti ya NMB kwenda akaunti ya Cariton Trading Co Industrial. Pia alihamisha tena Sh milioni 60.5 kwenda akaunti ya Jacques Investment.

Katika mashitaka mengine, Mtoro anadaiwa kutakatisha fedha haramu kwa kubadilisha fedha kwa kununua nyumba maeneo ya Mbezi. Anadaiwa kutakatisha Sh milioni 579,887,395 zilizohamishwa kutoka akaunti ya NMB kwa udanganyifu.

Inadaiwa sehemu ya fedha hizo alinunulia nyumba Mabibo. Kikopa anadaiwa kutakatisha Sh milioni 389 zilizohamishwa kutoka akaunti ya NMB na Mtoro kwenda akaunti ya Cariton ambayo yeye alikuwa mtiaji saini pekee.

Anadaiwa kutakatisha tena Sh milioni 60 na sehemu ya fedha hizo Sh milioni 449 alinunulia nyumba maeneo ya Mbezi Mshikamano. Washitakiwa wote wanadaiwa katika kipindi hicho waliisababishia NMB hasara ya Sh 1,029,454,383.

Wote walikana mashitaka na Hilla alidai upelelezi umekamilika na kuomba tarehe ya usikilizwaji wa awali. Kesi hiyo itasikilizwa Agosti Mosi mwaka huu.

UJENZI  na ukarabati wa Soko la Kariakoo jijini ...

foto
Mwandishi: Flora Mwakasala

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi