loader
Wafurahishwa na kuendelea kwa miradi ya barabara

Wafurahishwa na kuendelea kwa miradi ya barabara

Pia wameiomba Serikali kutenga fedha zaidi ili ujenzi wa miradi hiyo mitatu ya barabara kwa kiwango cha lami inakamilika kwa wakati kwani kiasi kilichotengwa ni kimeonekana ni kidogo.

Miradi hiyo mitatu ni pamoja na barabara inayounganisha Mji wa Sumbawanga na bandari ya Kasanga mwambao mwa Ziwa Tanganyika ikipitia mjini Matai Makao Makuu ya Wilaya mpya ya Kalambo yenye urefu wa kilomita 112 .

Mradi huu unajengwa na Mkadandasi China Railway 15 Bureau Group Corporation (CR15G). Mingine ni barabara kutoka mji wa Sumbawanga kupitia Chala hadi Kanazi ya umbali wa kilomita 75 ikijengwa na mkandarasi Jiangxi Geo - Engineering (Group) Corporation na barabara inayounganisha kijiji cha Kanazi na mkoa wa Katavi yenye umbali wa kilomita 76 inayojengwa kwa kiwango cha lami ChinaHunan Construction Engineering Group Corporation.

Miradi yote hii mitatu kwa mujibu wa Meneja wa Tanroads Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Florian Kabaka inafadhiliwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100.

Pongezi za wakazi hao wa mikoa hiyo miwili imetokana na kauli ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Rukwa, Hypolitus Matete alipowahakikishia hivi karibuni kuwa Serikali tayari imetenga kiasi cha bilioni 19 ili kazi ya ujenzi wa miradi hiyo ya barabara kwa kiwango cha lami ianze tena.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Sumbawanga

Post your comments