loader
Wajawazito wawili wauawa

Wajawazito wawili wauawa

Aliyeuawa na mumewe ni Pendo Bwire (37) ambaye mauaji yake yalifanyika katika Kijiji cha Bugula.

Inadaiwa mumewe, Kenedy Msita (45) alimshambulia kwa kisu na shoka katika kile kinachodaiwa ni wivu wa mapenzi.

Baadhi ya majirani walioshuhudia tukio hilo, walidai jitihada za kuokoa maisha ya mwanamke huyo zilikwama baada ya mumewe kuwatisha kwa shoka na kisu alivyotumia kumshambulia mkewe hadi akapoteza maisha.

Watoto wawili wa familia hiyo, Anastazia Ludovic na Jenifa Kenedy katika maelezo yao, walidai kabla ya baba yao kuchukua hatua hiyo, kulikuwa na vurugu akimtuhumu mama yao kupata mimba nje ya ndoa.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, Pendo alichomwa kisu sehemu mbali mbali za mwili, kabla ya kukatisha maisha yake kwa kukatwa na shoka na kutenganisha kiwiliwili na kichwa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Valentino Mulowola, alisema mtuhumiwa huyo alijaribu kujiua baada ya kutenda kosa hilo, lakini alikamatwa na kwa sasa anaendelea kupata matibabu katika hospitali ya wilaya ya Ukerewe.

Kwa mujibu wa kamanda, juzi saa 11 alfajiri mtuhumiwa alitumia kisu chake kujikata na kutoboa tumbo lake hadi utumbo ukatoka nje.

Anatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya kupata nafuu. Katika tukio jingine lililotokea pia juzi saa 2 usiku katika Kijiji cha Lutare, mjamzito Teopista Alistaliko (43) aliuawa kwa kunyongwa na watu ambao hawajafahamika.

Habari kutoka kijijini hapo, zilisema siku moja kabla ya mwanamke huyo kupatwa na mauti, akiwa na wanawe wawili alikwenda shambani kulima, lakini hakurudi nyumbani hadi mwili wake ulipokutwa umetelekezwa kichakani.

Wakizungumzia tukio hilo, watoto wake walisema hawaelewi aliyehusika na kifo cha mama yao, kwa sababu walimuacha shambani akiendelea na kilimo na wao walirudi nyumbani saa sita mchana kuandaa chakula.

Kamanda Mulowola alithibitisha tukio hilo, akisema mwanamke huyo amebakwa na kisha kunyongwa na watu wasiojulikana kisha mwili wake ukatelekezwa kichakani.

Hata hivyo, alisema tayari polisi inaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kuwapata waliotenda mauaji hayo ili wafikishwe katika mkondo wa sheria.

Vituo vya afya vyafikia 8461Idadi ya Vituo vya ...

foto
Mwandishi: Jovither Kaijage, Ukerewe

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi