loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wakandarasi waidai serikali bil 600/-

Wakandarasi waidai serikali bil 600/-

Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli aliyasema hayo juzi mjini hapa wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi kwa kipande cha kilometa 4.8 cha barabara inayoingia mjini Manyoni kinachojengwa kwa kiwango cha lami na Kampuni ya Ujenzi ya mjini Singida, Gopro Co. Ltd.

Dk Magufuli alilazimika kutoa maelezo hayo baada ya Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoa wa Singida, Leonard Kapongo kumweleza kuwa mkoa ulikuwa unadaiwa jumla ya Sh bilioni 45.5 na wakandarasi mbalimbali, jambo linalomnyima amani na uwezo wa kusimamia ipasavyo wakandarasi hao.

Aliyataja madeni yanayomkosesha amani kuwa ni pamoja na la mkandarasi anayejenga barabara ya Manyoni – Chaya kupitia Itigi anayedai Sh bilioni 39.9, mkandarasi wa daraja la Sibiti anayedai Sh bilioni 2.2 na wakandarasi wazalendo wanaodai Sh bilioni 3.4.

"Madeni hayo yanajumuisha deni la mkandarasi anayejenga barabara hii utakayoiwekea jiwe la msingi hivi punde ambaye hadi sasa anatudai Sh milioni 638," alisema.

Hata hivyo, Waziri Magufuli aliwahakikishia wakandarasi wote nchini wanaoidai Serikali kuwa watalipwa fedha zao hivyo wasiwe na hofu wala wasiwasi bali waendelee kuchapa kazi.

"Tajiri kuwa na madeni ni kawaida. Nchi zote tajiri au watu wote matajiri wanadaiwa, hivyo sio kitu cha kushangaza, isitoshe unapokuwa unadaiwa ndipo unapokuwa na akili ya kutafuta pesa,” alisema Dk Magufuli.

Aidha, Dk Magufuli aliahidi kumlipa mkandarasi wa kipande hicho cha barabara ndani ya wiki mbili ili aweze kukamilisha kazi hiyo katika muda uliopangwa. Muda huo ni Septemba mwaka huu. "Kutolipwa fedha kwa wakati isiwe sababu ya mkandarasi yeyote kufanya kazi. Ukikaa bila kazi vifaa vinakaa bure, mwisho utakula mtaji. Ninyi mnafanya biashara, lakini sio kwa kudai riba hata kama mkataba unasema hivyo," alisema na kuongeza: “Iwapo kuna mkandarasi atadai riba au ‘idle time’, sawa tutakulipa, lakini hatutakupa kazi tena".

foto
Mwandishi: Abby Nkungu, Manyoni

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi