loader
Wakili kizimbani kwa kumjeruhi 'housegirl'

Wakili kizimbani kwa kumjeruhi 'housegirl'

Rwechungura ambaye amenyimwa dhamana kwa kile kilichoelezwa ni kwa ajili ya usalama wake kutokana na wananchi wa eneo analoishi kuwa na hasira kwa kitendo anachodaiwa kufanya, alifikishwa mahakamani jana.

Alisomewa mashitaka na Wakili wa Serikali, Mohamed Salum mbele ya Hakimu Mkazi Suleiman Mzava.

Salum alidai Juni 11, mwaka huu, eneo la Boko Njiapanda, Yasinter alimjeruhi Marina Mathayo kwa kumpiga na waya wa kompyuta sehemu mbalimbali za mwili wake na kumpiga kichwani kwa kutumia jagi la kusagia matunda jambo lililomsababishia maumivu.

Mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo. Upande wa mashitaka ulidai upepelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Mahakama iliombwa izuie dhamana ya mshitakiwa kwa muda kutokana na taarifa walizopata kutoka kwa Mkuu wa Upelelezi wa Kanda ya Kinondoni kwamba hali ya majeruhi si nzuri na pia wananchi wana hasira naye.

Kesi iliahirishwa hadi Julai Mosi, mwaka huu itakapotajwa tena.

Vituo vya afya vyafikia 8461Idadi ya Vituo vya ...

foto
Mwandishi: Flora Mwakasala

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi