loader
Wakulima wa pamba wadai fidia

Wakulima wa pamba wadai fidia

Wakulima hao ambao walitumia mbegu hiyo isiyo na manyoya, baada ya bodi hiyo ya pamba kuithibitisha, wamedai kuwa, haikuota vizuri na hivyo kupata hasara. Wakulima hao waliodai fidia ni kutoka Geita, Simiyu, Mara, Mwanza na Shinyanga.

Wakizungumza kwenye kikao kilichoandaliwa na Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA), kwa lengo la kujadili juu ya kilichotokea kuhusu mbegu mpya ya Pamba Quton walidai kuwa bodi hiyo, ilithibitisha kuwa mbegu hizo zisizo na manyoya ndio zinafaa kulimwa na wakulima katika msimu wa mwaka 2013-14 ambazo pia viongozi wa serikali walikuwa wakisisitiza wakulima kuzilima.

Mmoja wa wakulima kutoka mkoani Mwanza Hamza Mdumilu, aliitaka bodi hiyo ya pamba kuwalipa fidia wakulima hao kutokana na hasara waliyoipata baada ya kutumia mbegu hizo ambazo hazikuota na kusababisha hasara ya mamilioni ya fedha kabla ya msimu wa kilimo (2014-15) haujaanza.

"Miaka yote tumekuwa tukitumia mbegu zenye manyoya na kupata uzalishaji mkubwa na tulipata faida kubwa na kusomesha watoto wetu na kuendesha familia bila matatizo, lakini hatujui shetani aliyeingia kwenye bodi ya pamba na kuzalisha mbegu mpya ya zao la pamba ambazo hazina manyoya na kututia hasara wakulima,” alisema mkulima Mdumila.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya (TCB), Gabriel Mwalo, alikiri kuwa mbegu hizo mpya zilikuwa na kasoro na baada ya kufanya uchunguzi ziligunduliwa kuwa na fangasi hivyo zisingeweza kuota.

Mwalo alisema kutokana na utafiti walioufanya Ukiriguru ambapo mbegu hizo za pamba huzalishwa waligundua kuwa zilipata kasoro kutokana na utunzaji wake ambapo mbegu zilizobaki katika msimu wa mwaka jana za manyoya zilichanganywa sehemu moja na mbegu mpya, hali iliyosababisha mbegu hizo kuingiliwa na wadudu na kushambuliwa viini vyake.

Alisema bodi hiyo kwa kushirikiana na Serikali imeshakaa na kufanya utaratibu wa kuwalipa wakulima waliopata hasara kutokana na kutumia mbegu hizo ili kutowavunja moyo.

Zao hilo ndilo lenye asilimia kubwa ya kuajiri wakulima zaidi ya 500,000 pamoja na ongezeko la pato la taifa.

Naye mgeni mwalikwa katika kikao hicho mwenyekiti wa wabunge Kanda ya Ziwa John Shibuda, ambaye pia ni mbunge wa Maswa, alisema Bodi ya pamba imegubikwa na usiri mkubwa, na kuahidi suala hilo kulifikisha kwa waziri mwenye dhamana.

Serikali ya Marekani kupitia Shirika la Misaada la taifa hilo ...

foto
Mwandishi: Kareny Masasy, Shinyanga

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi