loader
Wakulima wa vitunguu wataka soko nje

Wakulima wa vitunguu wataka soko nje

Wakizungumza na waandishi wa habari, wakulima hao walisema wanalima vitunguu kama zao la kibiashara, lakini hawaoni tija, kutokana na bei wanazouzia, kutokuwa na faida huku baadhi ya wafanyabiashara wakinufaika na mazao hayo.

Joseph Karoli, mkulima wa kijiji cha Ndekeli Kata ya Tongi, alisema vipimo vya vitunguu vinawanyonya, kutokana na vipimo hivyo kuwa vikubwa zaidi.

Aliongeza kuwa hata bei ya zao hilo, hupungua na kushuka thamani siku hadi siku.

“Wakulima wa vitunguu tunanyonywa, upimaji ni wa rumbesa ni mbaya, lakini bei pia haina mpangilio, tunaiomba Serikali itusaidie suala hili, tuweze kujikwamua na ikiwezekana tutafutiwe soko zuri nje ya nchi,” alisema Joseph.

Karoli Paul alisema Serikali inapaswa kuingilia kati ili kuwasaidia wakulima katika kuhakikisha wanapata soko zuri na la uhakika ili waweze kuuza vizuri zao hilo na kufanya mabadiliko ya kiuchumi, tofauti na sasa wengi huuza kwa bei ya hasara.

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, Mrcelina Mihayo, alisema watakaa na wataalamu wa bishara wa halmashauri hiyo ili kulifanyia kazi suala la kutafuta soko la wakulima hao wa vitunguu.

Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Bituni Msangi aliwahakikishia wakulima hao, kuuza kwa bei nzuri yenye manufaa kwao.

Alisema vipimo wanavyolalamikia, vitafanyiwa kazi mara moja na hatua kali za kinidhamu, zitachukuliwa dhidi yao watakaobainika kuvitumia.

foto
Mwandishi: Lucas Raphael, Nzega

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi