loader
Wakulima wahimizwa kutumia ardhi kujikwamua

Wakulima wahimizwa kutumia ardhi kujikwamua

Mmoja wa wakimbiza Mwenge wa uhuru kitaifa, Hamza Mahmoud alitoa ushauri huo jana wakati akikagua shamba la mkulima wa zao la ndizi katika kijiji cha Kasulo wilayani Ngara mkoani Kagera.

Ziara kwa mkulima huyo ni sehemu ya kupeleka hamasa ya mwenge kwenye ufunguzi wa miradi kunakofanywa na mbio za mwenge.

Mahmoud alisema kitendo cha mkulima kutumia mtaji wake wa ardhi na mifugo kidogo kuandaa shamba na kutoa mazao yenye soko katika wilaya nzima na mkoa ni jambo la kuigwa katika nchi.

Pia aliwapongeza wakulima wa migomba akiwemo Samweli Kapalala ambaye shamba lake lilionekana kuvutia viongozi wa ngazi mbambali nchini ambapo shamba hilo alilianzisha mwaka 2003 kwa kianzio cha ekari mbili ambapo sasa limefikia ekari 6.5 likiwa na miche 444 ya migomba.

Akisoma taarifa za mradi wa shamba hilo, Kapalala alisema katika shamba hilo hupanda migomba inayotoa ndizi aina ya nchakala na sehemu ya shamba amepanda migomba aina ya FIA 17& 23 kwa ajili ya biashara ambapo ameweza kufanikiwa kupitia na kutumia wataalamu wa kilimo.

Alisema pamoja na ukulima wake tangu kuanzishwa kwa shamba hilo hadi sasa lina thamani ya Sh milioni 250 lakini katika uzalishaji zimeshapatikana Sh milioni 375 ingawa changamoto ni ukosefu wa soko na ugonjwa wa unyanjano.

Kwa upandewa mkuu wa Wilaya ya Ngara, Costantine Kanyasu alisema kuwa Mwenge umezindua miradi saba katika wilaya hiyo ambayo imegharimu kiasi cha Sh bilioni 1.2.

UJENZI  na ukarabati wa Soko la Kariakoo jijini ...

foto
Mwandishi: Angela Sebastian, Ngara

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi