loader
Walioiba fedha za tumbaku watakiwa kukamatwa

Walioiba fedha za tumbaku watakiwa kukamatwa

Rais Jakaya Kikwete alitoa agizo hilo akizungumzia malalamiko ya wananchi wa Wilaya ya Namtumbo ya kuibiwa fedha zao za zao la tumbaku na kushindwa kulipwa kwa miaka miwili sasa.

Alisema viongozi hao ambao ripoti ya Mkuu wa Mkoa inaonesha kuwa walishiriki katika wizi huo, wakamatwe na kufikisha mbele ya sheria.

“Hawa watu wanawadhulumu watu. Wanawafanya kama watoto wadogo. Hili jambo lisipelekwe kwa Wizara ya Kilimo, Chakula na Maendeleo ya Ushirika ama kwa Mrajisi wa Vyama vya Ushiriki – ripoti ya Mkuu wa Mkoa ipelekwe polisi kwa hatua za kisheria. Siyo kazi ya Wizara ama Mrajisi kuamua nani ashitakiwe kwa wizi. Wezi wanashtakiwa na Jamhuri,” ameagiza Rais Kikwete na kuongeza: Alisema, “Na nyie wananchi acheni kuchagua wezi kuongoza ushirika. Mnachagua wezi na wakishawaibieni mnaanza kulaumu Serikali na CCM – badala ya kukabiliana na kukamata wezi, mnalifanya jambo hili suala la kisiasa.”

Aliwasisitiza kwamba Chama cha Ushirika ni chao na fedha zilizoibwa ni zao.

“Viongozi wa ushirika mmewachagua wenyewe, sasa kwa nini mnalaumu watu wengine. Mnaruhusu watu watakate kwa jasho lenu. Kataeni wizi huu na wafikisheni wezi Polisi… habari ndiyo hiyo.”

Alimwambia Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Saidi Mwambungu, ahakikishe leo anakamata wote walioshiriki na kuiba fedha hizo na akishindwa, amwambie.

Rais Kikwete alisema mkuu wa mkoa ana mamlaka ya kufanya hivyo na kwa kuwa aliunda tume (Mwambungu) na imeshampa matokeo ya uchunguzi, hana sababu ya kuendelea kunyamaza wakati watuhumiwa wapo.

UJENZI  na ukarabati wa Soko la Kariakoo jijini ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi