loader
Wanafunzi wapatiwa elimu ya kujikinga na kichocho

Wanafunzi wapatiwa elimu ya kujikinga na kichocho

Kazi za kukagua afya za wanafunzi ikiwemo kupata chanjo ya kulindwa na ugonjwa wa kichocho umeanza katika shule za msingi za Kilimahewa pamoja na Chaani mjini hapa.

Ofisa Mkaguzi wa Afya kwa wanafunzi kujilinda na ugonjwa wa kichocho, Ali Ali alithibitisha kufanyika kwa ukaguzi wa afya kwa wanafunzi wa shule za msingi.

“Tumeanza ukaguzi wa shule kuhusu ugonjwa wa kichocho ambao tumegundua kwamba umeanza kujitokeza kwa kasi,” alisema.

Akizungumza na wanafunzi katika shule ya msingi ya Chaani, Diwani wa kijiji cha Gamba mkoa wa kaskazini Unguja, Machano Fadhil Babla aliwataka wanafunzi wa shule kuacha kuoga katika mito ambayo ndiyo chanzo cha ugonjwa huo.

Ofisa wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Said Ali alisema utaratibu wa kutoa dawa kwa wanafunzi kujikinga na ugonjwa wa kichocho kwa kiasi kikubwa utasaidia kuimarisha afya za wanafunzi wa shule za msingi.

Alisema ugonjwa wa kichocho kwa wanafunzi wa shule za msingi kama utaachwa unaweza kusababisha madhara makubwa ikiwemo tatizo la uzazi kwa watoto wa kiume na wanawake.

Utafiti uliofanywa katika shehia 15 za Unguja na Pemba umegundua kwamba lipo tatizo kubwa la ugonjwa wa kichocho kwa wanafunzi wa shule zaidi za mkoa wa kaskazini Unguja.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso ...

foto
Mwandishi: Khatib Suleiman, Zanzibar

Post your comments