loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wanaharakati wasihi nafasi zaidi kwa wanawake

Wanaharakati wasihi nafasi zaidi kwa wanawake

Kutokana na uwiano huo, vyama vya siasa nchini vimetakiwa kutoa kipaumbele na kushirikisha wanawake katika kugombea nafasi mbali mbali za juu za uongozi katika vyombo vya uamuzi.

Mratibu wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa), Mzuri Issa alisema licha ya kuwepo nafasi za viti maalumu, uteuzi huo haujatosheleza kufikia malengo ya usawa wa kijinsia katika maendeleo.

“Kwa mfano alisema katika Baraza la Wawakilishi lenye wajumbe 82, ni 26 tu wanawake katika nafasi za viti maalumu huku watatu wakitoka katika majimbo ya uchaguzi,” alisema.

Aliendelea kusema, “Vyama vya siasa vinatakiwa kutoa kipaumbele kwa wanawake kugombea nafasi za uongozi katika majimbo ya uchaguzi.”

Alitoa mfano wa Chama cha Wananchi (CUF) kuwa hakijatoa kipaumbele kwa wanawake kugombea nafasi za uongozi kwani katika uchaguzi wa mwaka 2010 hakuna mwanamke aliyesimamishwa katika majimbo ya uchaguzi tofauti na CCM.

Mzuri alitaja nchi za Ulaya ikiwemo Denmark pamoja na Sweden ambazo zimetoa kipaumbele kwa wanawake kugombea nafasi za uongozi kiasi kwamba, kwa sasa hakuna nafasi zilizotengwa maalumu kwa wanawake.

Alitaja pia nchi za Afrika, hususani Ghana, Msumbiji, Afrika Kusini pamoja na Rwanda kwamba zimefanikiwa kwa asilimia 64 kwa wanawake kugombea nafasi za uongozi.

Tamwa inaendesha kampeni kuhakikisha vyama vya siasa vinatoa kipaumbele na nafasi kwa wanawake kushiriki katika uongozi.

foto
Mwandishi: Suleiman Khatib, Zanzibar

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi