loader
Wananchi waombwa kusaidia kulinda ndege

Wananchi waombwa kusaidia kulinda ndege

Huku wakikumbushwa kuwa maeneo ya ardhioevu ndio vyanzo vya maji ambayo yanafaa kwa matumizi ya kila siku ya binadamu, wanyama na ndege, hivyo maeneo hayo ni vyema yalindwe kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.

Msemaji wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Nurdin Chamuya alisema hayo jana wakati akizungumzia maadhimisho ya Siku ya Ndege Wahamao Duniani ambayo huadhimishwa kimataifa Mei 10 hadi 11.

Alisema kuna aina nyingi za ndege maji na wahamao, ambao wanahama kila mwaka kutoka sehemu moja ya dunia kwenda nyingine kutafuta malisho, maji, kukwepa hali mbaya ya hewa na kupata sehemu salama ya kuzaliana.

Alisema Tanzania ni nchi mojawapo yenye sehemu nyingi ambazo ni salama kwa mazalia ya ndege kama katika Ziwa Natron ni maarufu kwa mazalia ya ndege aitwaye heroe mdogo (korongo).

“Inakadiriwa kuwa asilimia 80 ya heroe mdogo kote duniani huzaliwa katika Ziwa Natron liliko Kaskazini mwa Tanzania, ziwa hilo ni kivutio cha utalii kutokana na ndege, wanyamapori na mandhari ya Ziwa,”alisema.

Alisema maadhimisho ya Siku ya Ndege Wahamao Duniani yalianza mwaka 2006 na mwaka huu wizara hiyo itafanya maadhimisho hayo Katika Eneo la Ramsar la Ziwa Natron lililopo mkoani Arusha, ambapo ni eneo lenye umuhimu wa ndege wahamao aina ya heroe mdogo.

UJENZI  na ukarabati wa Soko la Kariakoo jijini ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi