loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wananchi waunge mkono sheria mpya ya maslahi

Wananchi waunge mkono sheria mpya ya maslahi

Mapendekezo hayo ambayo yalianza kutolewa kwa wadau wa elimu ni mahsusi kwa ajili ya kutimiza maagizo ya Rais Jakaya Kikwete ambaye amekuwa akisisitiza kuwa lazima ifike wakati kwa viongozi wa siasa kutenganisha siasa na biashara.

Wakiwasilisha mapendekezo hayo, mtoa mada Gertrude Cyriacus alisema Tanzania iko katika mchakato wa kutunga sheria ya kudhibiti Mgongano wa Maslahi, jambo ambalo ni miongoni mwa matatizo ya kimaadili yanayozikumba nchi nyingi, ikiwemo Tanzania.

Alisema tatizo hilo linaathiri maendeleo ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni.

Alisema hali halisi na changamoto ya migongano ya kimaslahi ni pamoja na kupokea, kuomba au kutoa zawadi au fadhila yenye lengo la kushawishi kupelekwa miradi ya maendeleo katika eneo lolote pasipo kuzingatia vipaumbele vya Taifa, kujilimbikizia mali isivyo halali, kujihusisha katika shughuli za kibiashara ambazo zinashahibiana na kazi au majukumu ya kiongozi.

Sheria hiyo ikipita itawazuia viongozi na watumishi, familia au makampuni yao kuingia mikataba ya kibiashara na taasisi wanazozisimamia pamoja na kujihusisha katika shughuli za biashara ambazo zinashabihiana na kazi au majukumu yao au shughuli za kitaaluma ambazo zinaweza kuathiri utekelezaji wa majukumu yao kwa umma.

Itawazuia viongozi na watumishi kushiriki katika michakato ya kutoa maamuzi ya masuala waliyo na maslahi binafsi au maslahi ya familia zao hususan: Kushiriki katika michakato wa ajira unaohusisha familia, rafiki au ndugu, michakato ya ongezeko au maboresho ya maslahi katika nyadhifa zao na mengineyo.

Naamini wananchi wengi watakubaliana na mapendekezo hayo kwa lengo la kuboresha utumishi wa umma na kusababisha huduma kutolewa kwa usawa bila kiongozi kutumia cheo chake kwa maslahi yake na familia.

Ingawa kuna baadhi ya vipengele ambavyo vinaonekana kuwa na changamoto za hapa na pale ni vema kila mmoja atakayepata nafasi ya kuchangia mapendekezo hayo kufanya hivyo kwa nia ya kuhakikisha sheria hiyo kusaidia katika kuboresha maisha ya watu na kuondoa malalamiko kwa viongozi hao.

Pia kutokana na umuhimu wa sheria hii ni vema tume kuisimamia kwa lengo la kuboresha mapendekezo waliyotoa ili pale itakapopitishwa isiwe na malalamiko kwa wadau wa aina tofauti .

Pia ni vema kuhakikisha mchakato wake unaenda haraka kwa lengo la kuwawezesha viongozi wa utumishi wa umma wanatumia sheria hii kuongoza nchi hususan baada ya uchaguzi mkuu ujao.

Naamini kuwa mapendekezo haya yana malengo mazuri kwani yatasaidia kupunguza rushwa na upendeleo kwa viongozi wa umma kwani watabanwa na sheria na kusaidia nchi kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili.

TANESCO ni shirika la huduma lakini pia ni ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi