loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wananchi wavamia kituo cha polisi

Wananchi wavamia kituo cha polisi

Habari zaidi zinasema wanakijiji hao wanadaiwa kuvamia eneo la kituo hicho na kufanya uharibifu mkubwa kwa kuchoma moto pikipiki, mtambo wa kufua umemejua na kupanda juu ya paa la jengo la kituo hicho na kuling’oa huku wakivunja madirisha mawili.

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Mihayo Msikela alisema tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 2:00 asubuhi katika kijiji hicho.

Kamanda Msikela alifafanua kuwa wananchi hao pia walichoma pikipiki yenye namba za usajili T 342 CEX aina ya SNLG ambayo ni mali ya askari polisi No.H 925 PC Benjamini.

Alisema kuwa tukio hilo lilitokea baada ya askari huyo wa kikosi cha usalama barabarani kumkamata mwendesha pikipiki Sijaona Ally (30) mkazi wa kijiji hicho kwa makosa ya usalama barabarani.

Inadaiwa kuwa mwendesha pikipiki huyo alikaidi kutii amri ya polisi iliyomtaka kusimama na ndipo wakaanza kufukuzana na hatimaye mwendesha pikipiki huyo alimgonga askari mwingine mwenye Na G 1921 PC, Chale ambaye aliyejeruhiwa vibaya na kijana huyo naye kuanguka na kujeruhiwa ambapo wote wamelazwa katika Hospitali ya Serikali ya wilaya ya Tunduru.

Kamanda huyo alifafanua kuwa kabla hawajapelekwa katika Hospitali ya wilaya, majeruhi hao walipelekwa katika zahanati iliyopo kijijini hapo ndipo vurugu zilipoanzia, baada ya wanakijiji kumtaka askari aliyejeruhiwa asipewe huduma ya matibabu kwenye zahanati hiyo, wakidai kuwa askari wana sehemu zao za kutibiwa.

“Katika hali hiyo ya mvutano baina ya wanakijiji na askari polisi ilifanya wanakijiji hao kuchukua maamuzi ya kwenda kukivamia kituo cha polisi na kuanza kufanya uharibifu huo, ambao ulisababisha vurugu kubwa na polisi wa Kituo Kikuu cha Mji wa Tunduru kulazimika kwenda kuongeza nguvu,” alisema Msikela.

Alisema kuwa kutokana na tukio hilo mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa licha ya kuwa kikosi maalumu cha polisi kutoka polisi mkoa kinachoongozwa na Ofisa Upelelezi wa makosa ya jinai ya mkoa, Revocatus Malimi kimeshapelekwa na kinaendelea kuwasaka watuhumiwa.

Kamanda huyo aliwasihi wananchi waache kujichukulia sheria mkononi na badala yake wafuate taratibu za kisheria kwa kupeleka malalamiko yao ofisi husika kama wanaona kuna mahali askari amewakwaza.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Diwani wa Kata ya Lukumbule, Issa Kitumbi na watendaji wa Vijiji vya Mchesi Ali Mnandi na Omari Chowo wa Lukumbule walisema kuwa vurugu zilianza kujitokeza katika zahanati ya kata hiyo baada ya wananchi kupeana taarifa juu ya tukio hilo.

Alisema kutokana na hali hiyo ilimfanya muuguzi wa kituo hicho kuwafungia ndani Polisi na majeruhi hao na kupiga simu Kituo Kikuu cha Polisi Tunduru ili kuomba msaada wa kuwanusuru polisi wasishambuliwe na wananchi hao.

foto
Mwandishi: Muhidin Amri, Tunduru

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi