loader
Picha

Wanaume ondoeni hofu upimaji tezi dume

Aidha, majimaji hayo huzipa mbegu za kiume nguvu ya kusafiri kwenye uke hadi mirija ya uzazi tayari kupevusha yai la kike.

Inaelezwa kadiri mwanaume anavyozeeka, ni jambo la kawaida tezi dume kuongezeka ukubwa, kuvimba na kusababisha madhara.

Moja ya madhara ya tezi dume ni kushindwa kutoka kwa mkojo, mgandamizo kwenye kibofu, maambukizi katika njia ya mkojo na madhara katika figo au kibofu cha mwanamume.

Pia yapo madhara mengine ambayo ni damu kuganda, nimonia na mwanamume kushindwa kutoa shahawa kwenye uume. Hivyo, elimu juu ya ugonjwa huu inapaswa kutolewa licha ya kuwepo kwa upotoshaji unaofanywa juu ya vipimo vya ugonjwa huo.

Wanaume wengi wana tabia ya kudanganyana kuhusu upimaji tezi dume licha ya kuwepo taarifa kuwa namna ya upimaji umebadilika.

Udanganyifu huu umefanya mwitikio wa kupima tezi dume kama alivyoomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwa mdogo.

Inaelekea wanaume sasa hawataki kupima na kufanya jamii kushindwa kuzungumzia ugonjwa huu licha ya kutajwa kuua sana.

Najua serikali ina malengo ya kumaliza magonjwa yasiyoambukiza hasa kwa kutoa huduma ya upimaji wa magonjwa haya bure.

Ni muhimu kushiriki kuwapima wanaume na kutoa elimu ya vipimo sahihi vya ugonjwa huu ili kuwajengea wanaume, kujiamini na kushiriki kupima ugonjwa huu kwa hiyari.

Mwishoni mwa wiki, Makonda alisema ana mkakati wa kupima ugonjwa huu nyumba kwa nyumba baada ya utoaji chanjo ya mlango wa kizazi kwa watoto wa miaka 14.

Kauli hii ya Makonda ilizua mijadala katika mitandao mbalimbali ya kijamii wengi wakidai hawawezi kupima kutokana na upimaji unavyofanyika licha ya Mkuu huyo kutoa ufafanuzi kuwa upimaji umebadilika.

Minong’ono iliyozuka mitandaoni inaonesha dhahiri mwitikio wa kupima ni changamoto kutokana na maelekezo yanayotolewa kuhusu upimaji wa tezi dume unavyofanyika.

Sasa ni wakati mzuri wa Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kutoa elimu juu ya kipimo sahihi na madhara yanayoweza kuwapata.

Naamini kufanya hivyo kutasaidia kukuza mwitikio wa upimaji na kusaidia wanaume kujua mapema wana maambukizi au la.

Mwito wangu wanaume wajenge utaratibu wa kutembelea vituo vya afya ili kupata taarifa kamili ya kupima kuliko kusikiliza taarifa za mitaani zinazowakatisha tamaa na woga.

Ni vyema ukapata taarifa kutoka kwa vyanzo muhimu kuliko taarifa za watu ambao hata hawajui namna ya kupima na hata wao hawajawahi kwenda kupima ugonjwa huo.

Ni vyema ukaamua kwa kuwa afya yako iko mikononi mwako.

Ni muhimu kujua kinga ni bora kuliko tiba hivyo ukibainika mapema utatibiwa na kuendelea na maisha kuliko kusubiri hadi ugonjwa ukafika hatua mbaya.

KISWAHILI ni kati ya lugha kongwe na yenye historia kubwa ...

foto
Mwandishi: Sophia Mwambe

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi