loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wanaushirika waomba nafuu kodi ya TRA

Wanaushirika waomba nafuu kodi ya TRA

Wamesema hatua hiyo itaongeza mitaji, pia kutoa hamasa kwa wanachama kupata mikopo mingi zaidi itakayowasaidia katika shughuli za kiuchumi.

Meneja wa Saccos hiyo, Abbas Rajab akisoma taarifa ya Saccos kwa Rais Jakaya Kikwete, jana kabla ya kuizindua, alisema Saccos hiyo yenye wanachama 1,779 kati ya hao wanawake wakiwa ni 500 imefanikiwa kuwa na mtaji wa Sh bilioni 4.3 na mikopo iliyokopeshwa na kurejeshwa ni Sh bilioni 3.3 , wakati mikopo ya kiasi cha Sh bilioni 1.04 haijarejeshwa na wanachama.

Kwa mujibu wa meneja huyo chama kinajiendesha chenyewe bila kutegemea mikopo kutoka nje na kwamba hadi sasa kina mtaji wa Sh bilioni 1.4 zikiwa ni akiba, amana na limbikizo la ziada.

Hata hivyo, alisema kutokana na hayo, Saccos hiyo imepata mafanikio kupunguza kero mbalimbali za kiuchumi na kijamii na kutengeneza ajira kutokana na wanachama wake kununua magari 100, pikipiki 150 na kufungua maduka.

Kwa mujibu wa meneja huyo kuna changamoto kubwa kwa baadhi ya wanachama kutorejesha mikopo kwa wakati na tozo la kodi kubwa ya TRA ya asilimia 30 na kumwomba Rais kuwapatia majawabu ombi hilo.

Kwa upande wake, Rais Kikwete, kabla ya kujibu hoja hizo, aliwapongeza wananchi hao kwa kuanzisha Saccos ambayo inajitegemea kimtaji na kukopesha wanachama wake fedha nyingi.

Rais alisema utaratibu wa kuanzisha Saccos lilikuwa ni jambo zuri kwa kuwa ni chombo kinachoweza kumkomboa mwananchi wa kawaida kwani mabenki si rafiki wa watu masikini.

“Vyama hivi vimeanzishwa ili kumkomboa mtu wa chini kwani mabeki si rafiki yao na Saccos zina faida ya kuwawezesha wanachama kujikopesha kwa ajili ya maendeleo yao ya kukuza uchumi wa mtu moja mmoja na taifa,” alisema Rais.

Katika hotuba hiyo alikubali ombi lao kwa kuwapatia kompyuta hizo tatu na kuwasihi wanachama kujenga tabia ya kurejesha mikopo kwa wakati ili wanufaishe na wenzao.

Sehemu kubwa ya ulimwengu wa biashara uli dorora kutokana na ...

foto
Mwandishi: John Nditi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi