loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wanawake washauriwa kubadilisha mfumo wa biashara

Wanawake washauriwa kubadilisha mfumo wa biashara

Rai hiyo ilitolewa juzi na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sofia Simba wakati akizindua kampeni ya Wanawake na Uchumi inayoendeshwa na Kampuni ya kusaidia wanawake ya Angels Moment mjini hapa.

“Wanawake nawaomba mbadilishe mfumo wa kufanya biashara, weka rekodi hata kama una Bajaj ujue kiasi gani kimeingia na pia wekeni akiba unaweza kuumwa huna hata fedha ya kwenda kupata matibabu,” alisema Simba aliyemwakilisha waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Simba alisema kutokana na wanawake kuendelea kuelimishwa namna ya kujikomboa kiuchumi sasa hivi umaskini wa kipato nchini umepungua kwa kiwango kikubwa.

Aliitaka Angels Moment kufanya kazi na maofisa maendeleo ya jamii nchini kote kwa sababu wao ndo wapo kwenye ngazi za chini na wanawafahamu wanawake wenye mahitaji ya elimu ya kujikomboa naumaskini.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Angels Moment, Naima Malima alisema kampeni hiyo imeandaliwa ili kuwaonesha wanawake fursa za uwekezaji kwa kutoa elimu juu ya tathmini ya uwezo wa kifedha kwa mtu binafsi, usimamizi binafsi wa fedha, uwekezaji na ukusanyaji utajiri, mikakati ya kujipanua kibiashara na mpango wa kustaafu na kurithisha biashara.

Kampeni hiyo inatarajiwa kuanza Septemba mwaka huu na kudumu kwa mwaka mmoja ambapo itafanyika katika mikoa ya Pwani, Mwanza, Kigoma, Tanga, Ruvuma, Dodoma na Lindi. Kampeni hiyo itafanyika katika awamu tatu.

Sehemu kubwa ya ulimwengu wa biashara uli dorora kutokana na ...

foto
Mwandishi: Maulid Ahmed, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi