loader
Washauri uangalifu bidhaa za umemejua

Washauri uangalifu bidhaa za umemejua

Ushauri huyo ulitolewa na Meneja Masoko wa Kampuni Ensol inayotengeneza vifaa vya umeme wa jua, Samanchogu Kihore alipokuwa akizungumzia mtambo mpya wa nguvu ya jua asili kwa kuchemsha maji ya moto katika maonesho ya kimataifa ya sabasaba.

“Kwa sasa bidhaa feki ni nyingi mitaani hivyo lazima kuwa makini katika kununua hivyo ninaisihi serikali kuendelea kubana kwa kuwa na sheria kali ili kudhibiti vifaa hivyo,” alisisitiza.

Akizungumzia mtambo huo mpya katika maonesho hayo, alisema mtambo huo jua linapiga tu na maji yanachemka huku ikiwa na uwezo wa kuhifadhi maji hayo kwa saa 72 kwa lita 100 hadi 1,000 na kuwekwa katika hoteli, hospitali, nyumba za kawaida na nyinginezo.

Alisema mtambo huo unaouzwa kwa Sh 500,000 na kudumu kwa zaidi ya miaka 15 haitumii kemikali yoyote wala kielektroniki kwa ajili ya kutunza mazingira na kuokoa gharama.

WAKALA wa Usafi ri wa Mabasi ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko na Katuma Masamba

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi