loader
Washauriwa kuchangamkia hati fungani za Serikali

Washauriwa kuchangamkia hati fungani za Serikali

Hayo yalielezwa jana na Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Fedha wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Mohamed Kailwa, wakati alipofanya mahojiano na gazeti hili katika Viwanja vya Maonesho ya Nanenane vya Ngongo mkoani Lindi.

“Mkulima akishavuna mazao yake na kuuza, sehemu fulani ya fedha zake ananunua pembejeo, sehemu nyingine anaitenga kwa ajili ya mahitaji muhimu na ziada anashauriwa kuwekeza katika hati fungani za serikali ambazo zina manufaa makubwa,” alisema.

Alisema kwamba pale wakulima wanapopatwa na shida kabla hati fungani zao hazijaiva, wanaweza kuziuza katika Soko la Hisa.

Ofisa huyo alisema faida nyingine ya kununua hati fungani za Serikali, mbali na kwamba ni za uhakika katika kulipwa zinapoiva, zinaiwezesha Serikali kugharimia miradi ya maendeleo na kuwapelekea wakulima huduma mbalimbali za kijamii kama vile barabara, maji, huduma za afya na nyinginezo.

Alisema hati fungani za Serikali kwa anayenunua ni uwekezaji madhubuti ambao haumtupi muwekezaji.

Akifafanua, Kailwa alisema hati fungani za Serikali ambazo hutangazwa kila Jumatatu katika magazeti ya Daily News na Uhuru zimewaganyika katika makundi mawili; za muda mfupi na mrefu.

Dhamana za Serikali za muda mfupi ni zile ambazo zinaiva ndani ya mwaka mmoja, yaani siku 35, siku 91, siku 182 ama siku 364 na za muda mrefu ni zaidi ya mwaka mmoja. Kwa sasa dhamana za muda mrefu zipo za miaka 2, 5, 7, 10 na 15.

MGODI wa kati wa madini ya dhahabu ...

foto
Mwandishi: Hamisi Kibari

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi