loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wasiotumia leseni za madini kunyang'anywa

Wasiotumia leseni za madini kunyang'anywa

Hayo yalibainishwa mjini hapa jana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi wakati akiendelea na ziara yake ya kukagua miradi ya nishati na madini mkoani humo ambapo alitembelea maeneo mbalimbali ya wawekezaji wa madini aina ya gypsum na vitalu vya matoleo ya bomba la gesi linaloendelea kujengwa.

Alisema kwa taarifa alizopatiwa na idara ya madini Kanda ya Mtwara na Lindi, zaidi ya leseni 1,000 za uchimbaji zimetolewa kwa wachimbaji mbalimbali wa madini wakiwemo wadogo, wa kati na wakubwa lakini ni idadi ndogo ya leseni hizo hadi sasa ndio inayofanyiwa kazi.

“Nia ni kupunguza hisia kwamba kuna watu wanachukua leseni na kujilimbikizia bila kuzifanyia kazi, Sheria tunayo tutaitumia ipasavyo pale inapotakikana,” alisisitiza Maswi.

Kwa upande wake Kamishna wa Madini nchini Paul Masanja, alisema wizara hiyo imejipanga kuhakikisha inaisimamia ipasavyo Sheria hiyo ambapo kwa mwaka 2012 hadi 2014 pekee jumla ya wachimbaji wakubwa 463 na wadogo 621 walinyang’anywa leseni zao kutokana na kushindwa kuzitumia kwa muda unaotakiwa.

“Sheria iko wazi kila mtu anapewa leseni na anatakiwa aitumikie kwa miaka saba, na sisi tunachofanya ni lazima tunapotoa leseni tufanye ukaguzi ili kujua kama kweli leseni hiyo inafanyiwa kazi, maana kuna watu wana leseni za uchimbaji hadi 10 lakini wanafanyia kazi leseni mbili tu…hatutoi leseni hizi kwa ajili ya mtu kukaa nazo,” alisisitiza.

Naye Kamishna wa Madini Kanda ya Mtwara na Lindi, Benjamin Mchwampaka, alikiri kuwa katika eneo lake, wachimbaji wengi wa madini hasa ya gypsum wamekuwa wakihodhi leseni zaidi ya moja za uchimbaji lakini hawachimbi katika maeneo ambayo leseni hizo zinafanyia kazi.

Sehemu kubwa ya ulimwengu wa biashara uli dorora kutokana na ...

foto
Mwandishi: Halima Mlacha, Lindi

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi