loader
Dstv Habarileo  Mobile
Wataalamu wa afya kwenye mitaa wako wapi?

Wataalamu wa afya kwenye mitaa wako wapi?

Uwepo wa idadi hiyo unafanya kuwe na migahawa na hoteli nyingi, ambazo wananchi hujipatia huduma za vyakula na vinywaji. Mfano kwa wilaya ya Kinondoni pekee, migahawa au hoteli zinazotoa huduma hiyo ni nyingi, na hiyo nayo ni njia ya wamiliki kujipatia kipato kutokana na biashara inayofanywa.

Ni imani yangu kwamba wakati migahawa au hoteli husika inaanzishwa, ilipewa kibali au leseni ya kufanya biashara kwenye eneo hilo, na kwamba kwa mujibu wa kanuni na sheria za afya, eneo hilo limethibitishwa kufaa kwa matumizi hayo.

Na kwamba ni wajibu wa bibi na bwana afya wa wilaya husika, kukagua eneo maeneo hayo, kuona yanaridhisha kwa kutoa huduma hiyo.

Lakini kama ndivyo, hali sio nzuri hata kidogo kwenye maeneo mengi, mfano hata kwenye maduka ya dawa za binadamu au hata maduka ya kuuzia kitoweo (nyama), hali ni tete.

Mfano mzuri ni maeneo ya Sinza na barabara ya Tandale, kwa kweli hali ni mbaya, kwani migahawa na mabucha mengi yako kwenye mazingira hatarishi kwa afya za binadamu.

Cha kushangaza zaidi ni kwamba wakati mazingira machafu ndio yametawala, hakuna mtaalamu wa afya yeyote anayetembelea kufanya ukaguzi kujionea.

Matokeo yake wananchi wanakula kwenye mazingira hayo wakati mwingine kwa kutopenda, ila kutokana na hali halisi ya mazingira anayoishi inambidi ale.

Cha kushangaza zaidi ni hata pale ambako kuna mitaro ya kupitisha maji ya mvua, wenye migahawa hiyo wameibadilisha na kuwa mitaro ya kumwaga maji machafu ya chakula na taka za vyakula ambazo haziendi mbali, bali zinaoza na kutoa harufu kali inayoharibu mazingira jirani, yanayozunguka mgahawa au maduka hayo.

Tunajiuliza hivi hawa wataalamu wa mazingira na afya wako wapi? Kazi yao ni nini - ni kukaa ofisini na kusubiri kuletewa taarifa au kazi zao ni pamoja na kuzungukia maeneo hao na kukagua suala zima la usafi na mazingira?

Jambo hili la uchafu linakera, kwani wahusika au wasimamizi wake, wamelala na ndio maana hakuna anayejali hata hao wenye migahawa, maduka ya dawa na maduka ya kuuza nyama, hawaoni ni tatizo wao kumwaga maji machafu na taka mbele ya maeneo yao, tena uchafu huo unaachwa ukitoa wadudu na harufu kali, inayotokana na maji taka kutuama.

Ifike wakati kila mmoja atekeleze wajibu wake, kama wewe umepewa jukumu la kuhakikisha afya na mazingira kwenye eneo lako, basi eneo hilo linapaswa kuwa safi na ni lazima uwajibike kwa hilo.

Manispaa ya Kinondoni pamoja na nyingine, zina wajibu wa kuwajibika kwenye hili, kwani uchafu uliopo hivi sasa kwenye maeneo hayo ni kana kwamba hakuna wa kuuona.

Kwa Sinza, maeneo kuanzia Legho mpaka Afrika Sana, yanahitaji uangalizi wa wataalamu wa afya na mazingira, hasa eneo la Sinza Palestina, ambako kuna maduka mengi na migahawa pembezoni mwa barabara.

Eneo hilo la Sinza Palestina limekithiri kwa uchafu unaotupwa au kumwagwa kwenye mtaro wa maji ya mvua ulio jirani, ambao hivi sasa unatoa harufu kali. Vyombo husika visikie hili na kuchukua hatua, kwani ‘Mtu ni afya’.

TANESCO ni shirika la huduma lakini pia ni ...

foto
Mwandishi: Ikunda Erick

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi