loader
Wataka chombo maalumu kufumua mfumo dume

Wataka chombo maalumu kufumua mfumo dume

Kauli hiyo imetolewa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala, Dk Alexander Makulilo, wakati akizungumza kwenye mjadala kuhusu mchakato wa Katiba mpya.

Mjadala huo uliandaliwa na Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto(WLAC) kwa msaada wa shirika la kimataifa la OXFAM na kuwakutanisha wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini jijini Dar es Salaam.

Mhadhiri huyo alisema kwa muda mrefu kumekuwa na fikra potofu kwamba wanawake hawana uwezo ingawa kuna ushahidi wa wanawake ambao wamepewa nafasi na wamefanya vizuri.

Aidha, alisema utafiti uliofanyika mwaka 2013 na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kushirikiana na Taasisi ya Demokrasia (TCD), zimeonesha wanawake wanachagulika iwapo watagombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Kwa mujibu wa mhadhiri huyo, walibaini changamoto zinazowakabili wanawake kuwa ni mila na desturi na mfumo wa uchaguzi unawafanya baadhi yao kuhofia kusimama kuwania nafasi za uongozi na wanaume.

“Ukiangalia chaguzi zinatumia fedha nyingi na wanawake wamekandamizwa kiuchumi na hawana fursa kama walivyo wanaume na kwenye chaguzi kuna rushwa sasa wanawake unakuta hawana uwezo wa kutoa fedha kuwezesha kwenye kampeni kama wanaume,” alisema.

Mwanasheria wa WLAC, Faudhia Yassin, alilishukuru Shirika la OXFAM kwa kuwezesha mafunzo hayo kuwezesha wanafunzi kufahamu masuala mbalimbali ya Katiba iliyopo na rasimu mpya.

“Tumeshafanikiwa kuwafikia wanafunzi wachache lakini tunaamini kwa elimu waliyopata watawaelimisha wenzao na sisi tunaendelea kutoa fursa ya mafunzo kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali,” alisema Faudhia.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments