loader
Watanzania waishio nje wako tayari kuleta fedha

Watanzania waishio nje wako tayari kuleta fedha

Aidha, serikali imeshauriwa kuangalia upya utaratibu wa kutoa misamaha ya kodi, hasa kwa kampuni kubwa zisizohitaji msamaha huo, kuwezesha kuongeza pato la Taifa kama Watanzania wanavyobanwa kulipa kodi katika mataifa ya nje waliomo.

Hayo yalisemwa juzi na Mjumbe Kadari Singo, wakati akichangia mjadala wa Rasimu ya Katiba kuhusu Sura ya Kwanza na ya Sita.

Akitoa mifano ya mataifa mengine, Singo alisema ripoti ya fedha ya mwezi wa pili mwaka huu ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT), inaonesha kuwa Kenya inaingiza Dola za Marekani bilioni 1.7 kwa mwaka kutoka kwa Wakenya waliopo nje ya nchi hiyo.

“Nigeria diaspora inaingiza Dola za Marekani bilioni 21 ambayo kwa hapa nchini, kiasi hicho cha fedha kinaendesha Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kwa miaka mitatu. Uganda zinaingia dola za Marekani milioni 910 na China ni dola za Marekani bilioni 60 kwa mwaka,” alisema Singo.

Alisema Tanzania Diaspora inaingiza dola za Marekani milioni 10 hadi 37 kwa mwaka na kuwataka Watanzania kutopuuza raia walioko nje ya nchi, kwani wanaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza uchumi.

Singo alisema katika kuchangia katika pato la taifa, Uganda diaspora inachangia asilimia 4.3 wakati Lesotho inachangia asilimia 34.

Alilitaka Taifa kufikiria kwa kina kuhusu uraia pacha na kueleza kuwa Tanzania ni moja ya nchi saba pekee Afrika, zinazokataa uraia huo.

“Tusiwe wavivu kufikiria kuhusu uraia pacha, haki ya kuzaliwa kwa raia wa Tanzania walioko nje ni ya muhimu, viongozi wa Kitaifa wakija huko tuliko, tunawapokea na kuwazunguka kwa mazungumzo, leo tukija nyumbani tunaambiwa tumekimbia nchi, si kweli,” alisema Singo.HabarzotenaGloriTesha

foto
Mwandishi: Gloria Tesha na Ikunda Erick

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi