loader
Waziri aagiza PPRA kudhibiti manunuzi ya serikali

Waziri aagiza PPRA kudhibiti manunuzi ya serikali

Agizo hilo alitoa jana wakati akifungua warsha ya siku tatu ya Sheria ya ununuzi wa umma kwa Wakurugenzi wa Bodi,Wakuu wa taasisi na Mashirika ya umma na wakala wa serikali, inayofanyika jijini Arusha.

Alisema ni lazima kasi ya usimamizi wa matumizi hayo ikaongezeka, kwa sababu zaidi ya asilimia 70 ya bajeti ya maendeleo, asilimia 100 hutumika katika kufanya ununuzi, hivyo ni muhimu sekta hiyo ikawa na udhibiti mkubwa.

“Kila mmoja kwa nafasi yake anawajibu wa kuhakikisha kuwa kila ununuzi unaofanywa chini ya taasisi yake unafanywa kwa uadilifu na ufanisi mkubwa, ili fedha zinazotumika ziweze kuleta manufaa kwa walengwa,” alisema.

Saada aliagiza mamlaka husika kuwachukulia hatua kali na hasa wale wanaovunja sheria ya manunuzi ya umma ya mwaka 2011, ili fedha za wananchi ziwe salama na zifanye kazi iliyokusudiwa.

Aidha alisema kuna suala la gharama ambalo pia limekuwa gumzo kwa watu mbalimbali, kwamba utumiaji wa sheria ya ununuzi kwenye ununuzi huongeza gharama za ununuzi ukilinganisha na kufanya ununuzi kwa fedha tasilimu limetafutiwa ufumbuzi.

Ufumbuzi huo ni pamoja na kusisitiza wahusika kuzingatia ununuzi wa pamoja (Bulk Procurement) kutoka kwa wazalishaji badala ya wakala.

Saada alisema rushwa na ubadhirifu katika ununuzi vimekuwa vikiathiri sana sifa za nchi nyingi duniani na athari kubwa ni kutopatikana kwa matokeo yaliyokusudiwa na kuzijengea hofu kampuni zinazofaa kushiriki kwenye michakato ya zabuni ya nchi hizo.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa ununuzi wa umma (PPRA), Balozi Dk. Matern Lumbanga, alisema warsha hiyo imeandaliwa kwa lengo la kuwaelimisha walengwa kuhusu sheria ya ununuzi wa umma ya mwaka 2011 na kanuni zake za mwaka 2013.

foto
Mwandishi: John Mhala, Arusha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi